Header Ads Widget

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUHIMIZA AMANI

 

Mashekhe na viongozi wa dini wakiomba dua kuwaombea Viongozi na Walimu wa Dini waliotangulia mbele ya Haki sambamba na kuombea uchaguzi Mkuu uwe wa amaniNa Fadhili  Abdallah,Kigoma

KUELEKEA uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu Mwenyekiti wa Halmshauri kuu ya Baraza Kuu la waislam Nchini (BAKWATA) Shekhe Hamisi Mataka amewataka Mashekhe na viongozi wa dini kutumia nyumba zao za ibada na mikusanyiko ya kidini kuhubiri amani kuelekea kwenye uchaguzi huo.

Shekhe Mataka alisema kuwa hayo mkoani Kigoma katika Maulidi ya kuzaliwa Mtume Muhamad (SAW) yaliyoenda sambamba na kumbukumbu ya miaka 69 ya kifo cha Mwanazuoni mkubwa na Mwalim wa dini mkoani Kigoma, Shekhe Ibrahim Kabeke

Shekhe wa mkoa Kigoma Hassan Kiburwa akizungumza katika hauli ya kumbukumbu ya miaka 69 ya Mwanazuoni na Mwalim wa dini mkoani Kigoma Shekhe Ibrahim Kabeke

Mwenyekiti huyo wa Halmashaauri kuu ya BAKWATA alisema kuwa viongozi hao wa dini wanayo nafasi kubwa ya kupigania Amani na mshikamano wa nchi kwa kutumia nyumba za ibada na mikusanyiko ya kidini na kwamba kwa sasa ni muhimu kwa jambo hilo kufanyika kwa nguvu na kwa umoja wao.

Kwa upande wake Shekhe wa mkoa Kigoma, Hassan Kiburwa alisema kuwa Watanzania wanapaswa kuwa wamoja kila siku kama ndugu na wasikubali kutengenishwa na mambo ya kiduni ikiwepo kutaka kuwaingiza kwenye vurugu wakati huu wa uchaguzi Mkuu.

Shekhe wa mkoa  Mwanza Hassan Kabeke (aliyesimama) akizungumza jambo wakati wa Sherehe ya Maulid ya Mtume na kumbukumbu ya miaka 69 ya Mwanazuoni na Maalim Mkubwa wa dini Kigoma  Shekhe Ibrahim Kabeke

Akizungumzia Hauli hiyo ya Maulid Shekhe wa mkoa Mwanza,Hassan Kabeke alisema kuwa ni siku kubwa na adhimu ambayo inawarudisha waislam katika misingi ya kumjua Mungu kupitia mafunzo mbalimbali yaliyotolewa na Mtume Muhamad na Marehemu Shekhe Ibrahim Kabeke.

Pamoja na hilo Shekhe kabeke ameimiza waislam na Watanzania wote kujitokeza kwenda kupiga kura siku ya Oktoba 29 kuchagua kiongozi wanayemtaka huku akihimiza kura Amani na usalama vinapaswa kuzingatiwa na watu wote ili kuufanya uchaguzi wa Amani na salama ambapo dua ya kuombea uchaguzi na viongozi wa nchi ilifanywa.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI