Header Ads Widget

MNEC JUMA SIMBA GADAFFI AWANADI BUTEMBO UDIWANI MAGOMENI, TARIMBA UBUNGE KINONDONI

MNEC Dar es salaam Ndg.Juma Simba Gaddaffi akiwanadi Udiwani Ndg.Noordin Butembo (kushoto ) na mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni, Mhe Abbas Tarimba katika mkutano uliofanyika uwanja Deila Magomeni Makuti B, Oktoba 5,2025.


Na. Mwandishi Wetu, Dar es salaam.

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa (MNEC) kutokea Mkoa wa Dar es salaam ndugu Juma Simba Gadaffi amewanadi Wagombea wa Chama hicho akiwemo Mgombea Udiwani Kata ya Magomeni Manispaa ya Kinondoni Ndg.Noordin Butembo na mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni, Mhe Abbas Tarimba katika mkutano uliofanyika uwanja Deila Magomeni Makuti B, Oktoba 5,2025.

Akizungumza katika mkutano huo, MNEC Juma Simba Gaddaffi amesema kuwa, CCM ni Chama kikubwa kinachifuata misingi, hivyo Wananchi waendelee kuwa na imani na wajitokeze kwa wingi bila woga kupiga kura hiyo Oktoba 29, 2025.

"Tanzania inaongozwa na Sheria. Kuweni na amani na Oktoba 29 watu wajitokeze kwa wingi kupiga kura  nyingi za Ndiyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Mbunge Abbas Tarimba na Diwani Noordin Butembo.



Kwa upande wake, Mgombea Ubunge Jimbo la Kigamboni Ndugu Abbas Tarimba amewahakikishia Wananchi hao wa Magomeni kuwa, wakimchagua ndani ya siku 100 atapeleka fursa za mafunzo bora ya namna ya kupata kipato kupitia mikopo ambapo watu wote wakiwemo akina Mama, Vijana na makundi maalum.

"Fursa hii inakuja kwenu,  tunahitaji Mbunge shupavu Kinondoni ambaye ni Mimi Tarimba, na Diwani Noordin Butembo wa Magomeni na Rais Samia Suluhu Hassan.

Tarehe 29 ndo siku ambayo tunaenda kupiga kura, nchi hii ni huru, kila anayetaka Uongozi, anatakiwa aletwe kupitia sanduku la kura. Kila mmoja wetu tujitokeze kwenda kupiga kura kwa wingi ya Ndiyo kwa wagombea wa CCM.




"Twende tukamchague Samia Suluhu Hassan, pia mkanichague mimi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni na kwa hapa Magomeni, mchugueni Noordin Butembo". Amesema Abbas Tarimba.

Kwa upande mgombea Udiwani wa Kata hiyo ya Magomeni, Noordin Butembo amewataka Wananchi wa Magomeni kuendelea kuwa na imani na CCM na ameomba wamchague tena kwa kura nyingi ilikuendelea kutimiza asilimia iliyobakia katika masuala mbalimbali ikiwemo Miundombinu, elimu, Afya na mengine katika Jamii ya Magomeni.











Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI