Header Ads Widget

TUMERIDHISHWA NA MRADI WA JENGO LA CHUO CHA MWEKA: MHE. MNZAVA



Na. Sixmund Begashe, Moshi.


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imeridhishwa na ujenzi wa mradi wa jengo la Taaluma la Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka na kuipongeza Serikali kwa kazi nzuri ya kuboresha miundombinu ya chuo hicho.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge  Ardhi Maliasili na Utalii Mhe. Timotheo Mnzava (Mb), Wilaya ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro, kwenye ziara ya kamati hiyo iliyo lenga kujionea ujenzi wa mradi .

Mhe. Mnzava amesema kuwa, wamejionewa namna Chuo hicho kilivyo na umuhiku mkubwa katika Uhifadhi wa Maliasili nchini hivyo ni vyema Serikali ikaendele kuboresha zaidi miundombinu yake na ya vyuo vingine chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii. 

Akizungumza baada ya ziara ya Kamati hiyo ya Bunge, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), ameshukuru kwa maoni yote yaliyotolewa na wajumbe wa Kamati, kwa kuwa yatasaidia Wizara hiyo kuinua zaidi uwezo wa vyuo chini ya Wizara hiyo. 

Dkt. Kijaji ameihakikishia Kamati hiyo kuwa itatekekeza maelekezo yote ambayo kimsingi yameonesha  dhamira ya dhati ya kuunga mkono juhudi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ni Mhifadhi namba moja ya kuhakikisha chuo hicho kinaendelea kutoa elimu bora zaidi na kuchangia uhifadhi endelevu wa Maliasili. 

Aidha. Dkt. Kijaji amebainisha kuwa jitihada zinanoendelea  kukiboresha Chuo hicho chenye kazi kubwa ya kuwaandaa wahifadhi bora nchini, zimepelekea Chuo hicho kukimbiliwa na wanafunzu kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni. 

Akizungumza baada ya kikao cha Kamati hiyo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu,  Dkt. Kijaji licha ya kuupongeza uongozi wa Mkoa huo kwa kazi nzuri ya uhifadhi, ameahidi kuwa Wizara hiyo itaendelea kushirikiana na uongozi wa Mkoa na wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa maslahi mapana ya Maliasili na Utalii nchini. 









Ziara hiyo imehudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Godfrey Mnzava, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi, baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara na  uongozi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania Mwemaka.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI