Header Ads Widget

BREAKING:MOTO WATEKETEZA MADUKA YA VINYAGO IRINGA MASAI MARKET

 

TAZAMA FULL VIDEO TUKIO LA MOTO IRINGA MASAI MARKET BOFYA LINK HII

Na Matukio Daima Media 

MOTO Mkubwa ambao chanzo chake bado kujulikana umeteketeza maduka zaidi ya 20 ya wafanyabiashara wa vinyago eneo la Iringa Masai Market ndani ya Bustani ya Manispaa ya Iringa. 

Matukio Daima Media imefika eneo la tukio la kuzungumza na mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo wafanyabiashara wa eneo hilo lililoteketea kwa moto ambao wamedai chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.

 

Rasi Kibodya alisema kuwa katika tukio hilo hakuna Mali hata moja aliyofanikiwa kuokoa. 


Mwenyekiti wa eneo hilo la Iringa Masai Market Mussa Onesmo alisema kuwa alipigiwa simu na mlinzi wa eneo hilo kumjulisha tukio hilo la moto na alipofika alikuta moto tayari umeweka vibanda kadhaa vikiwa vimeshika moto na ndipo alipokimbia hadi ofisi za Zimamoto umbali wa mita zaidi ya 500 kutoka eneo hilo kwenda kutoa taarifa. 


"Nashukuru baada ya kafika ofisi za Zimamoto walifika haraka eneo la tukio japo tayari moto ulikuwa umechukua kasi maana maduka yetu yote yalijengwa kwa mbao na miti hivyo moto ulikuwa unashika kwa kasi"

Hata hivyo alisema eneo hilo lina maduka zaidi ya 50 Ila kati ya hayo maduka zaidi ya 20 ndio yameteketea na maduka. 

Alisema moto huo ulianzia duka namba 7 ambalo kimsingi huwa hakuna shughuli yoyote ya moto zaidi ya kuwasha taa na kuzima na kuwa eneo hilo hakuna mgahawa wala shughuli inayotumia moto. 

Alisema sehemu kubwa ya waliopoteza Mali katika tukio hilo la moto wana mikopo ya taasisi mbali mbali za kifedha na wengine mikopo asilimia 10 ya Halmashauri na wengine ni mitaji binafsi. 


Yohana Ng'eng'ena ni mkurugenzi wa studio ya picha ya Mgonanzi alisema studio yake ni kati ya maeneo yaliyonusurika kweni ipo mita 10 ama 15 toka maduka mengine yalipoteketea.

Kuwa katika tukio hilo anamshukuru Mungu moto haukufika eneo lake hivyo hakuna Mali iliyoteketea. 


Mstahiki Meya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akiwa ameongozana na viongozi wengine wa CCM wilaya ya Iringa mjini mbali ya kutoa pole kwa wafanyabiashara hao alisema Hadi sasa wanagonjwa tathimini ili kujua madhara zaidi. 


Mkuu wa wilaya ya Iringa Benjamin Sitta ametoa pole kwa wafanyabiashara wote na kuwa serikali inaendelea kufuatilia zaidi ili kujua chanzo cha moto huo pamoja na hasara iliyojitokeza.

Sitta ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Iringa alisema jitihada kubwa zimefanyika na jeshi la Zimamoto na uokozi Iringa pamoja na jeshi la polisi katika kukabiliana na janga hilo la moto.

Hata hivyo alisema baada ya uchunguzi na tathimini atatoa taarifa nzima ya tukio hilo pamoja na kujua idadi kamili ya waliopoteza Mali zao.

Jackline Mtei ni kamanda wa Zimamoto na uokozi mkoa wa Iringa alisema kuwa moto huo umetokea kati ya saa 4 usiku kuelekea saa 5 usiku Jumapili machi 15 mwaka huu na kuwa chanzo bado hakijafahamika na kuwa wanaendelea na uchunguzi asubuhi. 

Hata hivyo aliwaomba wananchi kutumia namba ya 114 kupiga simu badala ya njia iliyotumiwa na wafanyabiashara hao kukimbia  hadi kituo kutoa taarifa kumbe wangepiga simu gari zingefika kwa wakati






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI