Header Ads Widget

PWANI IONGOZE KWA KURA ZA RAIS DKT SAMIA NCHINI - ALHAJI DKT. TINDWA.

 

Na matukio daima media

MJUMBE Kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Alhaji DKT. Chakou Khalfan Tindwa amewataka wananchi wa mkoa wa Pwani kujazia kura nyingi za kutosha mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dkt Samia suluhu Hassan ili mkoa huo uongoze kitaifa kwa idadi kubwa ya kumpigia kura nyingi nchini.

Amesema hayo wakati akihutubia wananchi wa Kata ya Makurunge iliyopo Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani kumuombea kura za kishindo kutoka kwa wananchi waliojitojeza leo kwenye ufungaji wa kampeni ambapo pia akimnadi mgombea wa kiti cha Ubunge wa jimbo hilo Dkt. Selemani Jafo ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara pamoja na Diwani Wakili Msomi Aidan Kitale.

Dkt. Tindwa aliwaomba wananchi kutumia haki yao ya kikatiba ya kujitokeaza kwa wingi katika vituo vya kupuiga kura siku ya juma tano tarehe 29 Oktoba 2025 kwa kumchagua kwa kura nyingi Mgombea huyo wa CCM ilia pate kura nyingi za kutosha kuliko mikoa yote nchini.

Alisema “katika historia miaka yote Mkoa wa Pwani umekua ukishika nafasi ya tano kwenye matokeo ya uchaguzi mkuu, kwa mwaka huu ikibidi Mkoa ukashike namba moja na anaimani kwamba itawezekana”. 
"Namuombea kura mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kiti cha Rais , pia namuombea kura Dkt. Selemani Jafo anayewania kiti cha Ubunge na Udiwani Wakili Msomi Aidan Kitale" alisema.

"Ifikapo tarehe 29 Oktoba Mwaka huu (Mtondo) kahakikisheni mnakwenda kupiga kura na usitoke pekeako toka na familia yako na mkaichague CCM kwa sababu ni Chama chenye uzoefu wa kuongoza ili wote mkachague mafiga matatu ya Chama Cha Mapinduzi ambayo (CCM),ambayo ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wetu Dkt. Selemani Jafo na Diwani Wakili Msomi Aidan Kitale" amesema Dkt. Tindwa.
"Makurunge ni kati ya maeneo kumi bora ambayo yamefikiwa na umeme ndani ya jimbo hili , mwezi uliopita nilikua nchini Zambia vijijini kwenye shughuli zangu sina budi kusema nchi yetu iko mbali katika masuala miundombinu kama umeme, barabara na afya ukilinganisha na nchi za jirani na hii yote inatokana kuwa na Uongozi madhubuti wa CCM hivyo ni jambo la kujivunia" amesema Dkt. Tindwa.

Naye Katibu Kamati ya Mikakati UWT Kanda ya Mashariki Mhe.Hawa Abdulrahman Ghasia amewaeleza wananchi wa Makuringe kamwe wasitishike na kauli zinazotolewa na baadhi ya watu kwamba siku hiyo kutakua na fujo.

"Kamwe msitishike na Kauli za mitandaoni hakuna kitu kibaya kitakachotokea kwani miongoni mwa wagombea wenye uzoefu kuliko wote ni mgombea wa kiti cha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa CCM, yeye anajua kila anachokiomba kwa wananchi tofauti na wagombea wengine ambao uzoefu wao ni kutoa lugha za kebehi, matusi, maandamano na kulala gerezani tena huku familia zao zikiwa ziko nje ya nchi" amesema Ghasia.


Mgombea kiti cha Ubunge Dkt. Jafo amewasisitiza wananchi wa Makurunge Jimboni Kisarawe kujitokez kwa wingi kwenye siku ya uchaguzi na kusisitiza wamchague Mhe.Rais Dkt. Samia yeye Mbunge wa Kisarawe na Diwani wa Kiluvya Kitale. 

Kitale amesema kuwa anatoa shukrani kwa timu ya kampeni Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani huku akiomba kura za mafiga matatu ambazo ni nafasi ya Rais, Mbunge na Diwani.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI