Header Ads Widget

''NINA WATOTO WAWILI WALEMAVU, SASA MNANIPEKEA WAPI''-MAMA AMINA (72).

 

Morogoro

MWANAMKE mmoja mwenye umri wa miaka 72, Amina Agustino mkazi wa Mtaa wa Nguzo,kata ya Mazimbu manispaa ya Morogoro, amefunguka kwa majonzi baada ya nyumba anayoishi kutangazwa kuuzwa kwa mnada kufuatia maamuzi ya Mahakama yaliyompa ushindi mumewe wa zamani Juma Khalifani katika kesi ya talaka.

Amina, anayelea watoto wawili wenye ulemavu,mmoja ulemavu wa akili na mwingine wa viungo, amesema hana pa kwenda endapo mnada uliopangwa kufanyika Novemba 7, 2025 utafanyika kama ilivyotangazwa na kampuni ya udalali wa mahakama Shashinhale Auction Mart.

 “Naomba Serikali inione tu kwa jicho la Kipekee, sina pa kwenda na hawa watoto wangu wenye ulemavu wananitegemea mimi kwa kila kitu, saa 24 zote, umri nao umeshanitupa mkopo” amesema kwa sauti ya huzuni.


Mwenyekiti wa mtaa huo, Daniel Kamili, amesema ofisi yake inafahamu mgogoro huo na ilijaribu kushauri awali Bila mafanikio.

Akamuomba Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na mamlaka zake  za juu kuingilia kati ili mama huyo asiwe katika hatari ya kukosa makazi pamoja na watoto wake wenye ulemavu.

Matukio Daima imefika eneo la tukio na kukuta karatasi za notisi zikiwa zimebandikwa maeneo mbalimbali zikitoa siku 14 ili nyumba hiyo ipigwe mnada.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI