Header Ads Widget

JESHI LA UHIFADHI LAPATA NGUVU MPYA, MAAFISA NA ASKARI 680 WAHITIMU WAFUNZO YA NADHARIA NA VITENDO KATAVI


Na. Edmund Salaho /Mlele-Katavi

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas amefunga rasmi mafunzo ya nadharia na vitendo ya Uongozi kwa Maafisa na Askari 311 wa Jeshi la Uhifadhi kutoka TANAPA na Mafunzo ya Awali ya Askari 369 wa TFS leo,  Oktoba 25, 2025 katika Chuo cha Mafunzo cha Jeshi la Uhifadhi Mlele mkoani Katavi.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Dkt.Hassan Abbas aliwataka wahitimu hao kutekeleza mafunzo waliyoyapata kwa

vitendo, kushirikiana kazini, na kuongeza uwajibikaji ili kuleta tija kwa Taifa.

Awali, Dkt. Abbas alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa ajira kwa vijana wa Tanzania katika sekta ya Maliasili na sekta zingine nchini.


"Tumshukuru Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kibali cha kuajiri Askari 311 na wengine zaidi ya 500 wanaokuja kupata mafunzo hapa pamoja na kuruhusu kupandishwa vyeo kwa Maafisa na Askari na niwatake vijana nchini kuchangamkia fursa ya ajira zinazotolewa katika sekta ya Maliasili na sekta zingine ambazo zinaendelea kutolewa na serikali".

Naye, Kamishna wa Uhifadhi, TFS - Prof. Dos Santos Silayo aliwapongeza wahitimu hao kwa kumaliza mafunzo yao na kuwataka kutumia mafunzo waliyoyapata katika kuendeleza sekta ya Uhifadhi na Utalii nchini.

Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara TANAPA, Massana Mwishawa alibainisha kuwa mafunzo waliyopatiwa Maafisa na Askari yanawajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku katika kuhifadhi Rasilimali za Wanyamapori na Misitu nchini.

"Mafunzo yanayotolewa hapa Mlele yanawajengea uwezo Maafisa na Askari wa Jeshi la Uhifadhi katika kutekeleza jukumu la ulinzi wa rasilimali za Taifa kwa niaba ya watanzania. Sisi kama viongozi wao tunaahidi kuwasimamia vyema na kwenda kutimiza kiapo chao kwa asilimia mia moja."

"Mafunzo haya ni muendelezo wa Jeshi letu kuimarika kwa ushirikiano na Jeshi la Wananchi (JWTZ), Jeshi la Polisi,na vyombo vingine vya Usalama ni ahadi yetu kuwa tutafanya kazi usiku na mchana ili kulinda Maliasili na kuboresha huduma kwa watalii wanaotembelea maeneo yetu ya vivutio" alisema Kamisha Mwishawa












Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI