Header Ads Widget

JAFARRY NYAIGESHA AHITIMISHA KAMPENI ZA CCM KATA YA UBUNGO, AWAHAKIKISHIA WANANCHI KUKAMILISHA MIRADI ILIYOBAKI

Mgombea Udiwani wa Kata ya Ubungo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Jaffary Nyaigesha (kushoto) akinadiwa na mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo Profesa Kitila Mkumbo leo Oktoba 27, 2025


Na. Mwandishi Wetu, Ubungo.

MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Ubungo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Jaffary Nyaigesha amehitimisha kampeni zake kwa kishindo zilizofanyika katika uwanja wa Millard Ayo (Uwanja wa Maji soda) Mtaa wa Msewe, Oktoba 27, 2025.

Katika mkutano huo licha ya mvua za hapa na pale, Wananchi wa Kata ya Ubungo wameweza kujitokeza kwa wingi kusikiliza sera za Nyaigesha ambaye anaomba nafasi hiyo kwa mara pili ili aendelee kuwatumikia.

Aidha, katika mkutano huo, Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo la Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo alipata wasaha wa kumnadi na kumuombea kura mgombea Urais wa Chama hicho, Mhe Samia Suluhu Hassan, pamoja na kura, Diwani na yeye kama Mbunge ili kupata mafiga matatu.


Kwa upande wake, Mhe Nyaigesha amewaomba kura nyingi za Ndiyo Wananchi wa Ubungo ili aendelee kuwatumikia ikiwemo kuendeleza miradi iliyobakia na mipya.

Katika kunadi sera katika mkutano huo wa kufunga, amesema miradi mbalimbali imefanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya CCM ikiwemo shule, huduma za Afya na miundombinu katika mitaa yote ya Kata hiyo.

Ambapo pia amewahakikishia suala la Usalama kwani Wananchi wajitokeze kwa wingi bila kuogopa ilikupiga kupiga kura za kishindo kwa Chama Tawala.








Mgombea Udiwani wa Kata ya Ubungo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Jaffary Nyaigesha akinadi sera katika mkutano wa kufunga kampeni leo Oktoba 27, 2025


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI