Header Ads Widget

DHAHABU YAPANDA NA KUWEKA REKODI YA DOLA ZA MAREKANI BILIONI 4.3 KATIKA SOKO LA DUNIA


Kwa mujibu wa ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya mwezi Septemba 2025 imeeleza kwamba rekodi ya  madini ya dhahabu  imepanda hadi kufikia dola za Marekani bilioni 4.3 katika soko la dunia.

Ripoti ya BoT  imeeleza kwamba, uuzaji wa bidhaa za huduma nje ya nchi umeongezeka kwa asilimia 14.8 kwa mwaka na kufikia jumla ya dola za Kimarekani 16,894.4  mwishoni mwa mwezi Agosti 2025.

BoT imefafanua kuwa , kwa upande wa uuzaji wa dhahabu uliongezeka kwa asilimia 35.5 na kufikia dola milioni 4, 322.3 kutokana na kupanda kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia.


Ikielezea kuhusu mauzo ya  bidhaa kutoka Sekta ya Kilimo ripoti imeeleza kuwa, katika mwezi husika mauzo yaliongezeka hadi kufikia dola milioni 1,411.7 ambapo ongezeko hilo ni sawa na asilimia 28.3 lililotokana na mauzo ya korosho , tumbaku na kahawa.

Pamoja na dhahabu mauzo  mengine ni bidhaa za viwandani, korosho Tumbaku na nafaka.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI