Header Ads Widget

ENG. KUNDO ASIMAMISHA SHUGHULI BARIADI MJINI AKIMNADI DK. SAMIA.


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Bariadi Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhandisi Kundo Mathew (wa tatu kulia) akiwa na viongozi mbalimbali pamoja na wanaCCM wakishiriki matembezi kuelekea Uwanja wa Salunda Shule ya msingi mjini Bariadi Kwa ajili ya Mkutano wa kampeni.

Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi-Simiyu.


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Bariadi Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhandisi Kundo Mathew amesimamisha Shughuli mjini Bariadi Mkoani Simiyu, akimnadi Mgombea Urais Dk. Samia Suluhu Hassan na kuwataka wanachi kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, 2025.


Katika maandamano yaliyoongozwa na Waendesha Bodaboda, daladala za Baiskeli, Guta za Pikipiki pamoja na Watembea kwa miguu, yalianzia uwanja wa CCM mjini Bariadi kuelekea kwenye Mkutano uliofanyika Salunda Shule ya Msingi yakifunga barabara kuu (Somanda-Luguru) kwa muda.



Akizungumza kwenye Mkutano huo, Mhandisi Kundo amewataka wananchi kuchagua Wagombea wa CCM sababu wanatoka Chama ambacho Mipango yake inaweza kutekelezeka.


Amesema kuwa, CCM inahitaji watu wanaobeba agenda za CCM kwa ngazi ya Urais ni Dk. Samia Suluhu Hassan mwenye dhamira ya kweli na amebeba matamanio ya Watanzania ambayo yameonekana kwenye Barabara, Afya, Mawasiliano, Umeme, Maji na Elimu.


"Jukumu la CCM ni Utekelezaji wa Ilani, hata tusipokuwa na mshindani, mshindani wetu ni Ilani ya CCM ambayo ni mkataba wa wananchi na Chama Cha Mapinduzi ambao umebeba matamanio na mahitaji ya wananchi...nawashawishi Wana Bariadi tukampigie kura Dk. Samia sababu alikuja akaahidi soko na limeanza kujengwa" amesema.



Mwisho.






















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI