Header Ads Widget

ENG. KUNDO ACHAMBUA ILANI YA CCM AKIMWOMBEA KURA DK. SAMIA.

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Joshua Mirumbe (kulia) akimkabidhi Ilani ya CCM 2025/2025, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bariadi Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi, Mhandisi Kundo Mathew kwenye Mkutano uliofanyika Salunda Shule ya msingi.


Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Bariadi mjini, Mhandisi Kundo Mathew amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, 2025, kumpigia kura Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuchapa kazi sababu anatekeleza miradi ya Maendeleo kwa vitendo.


Mhandisi Kundo ameyasema hayo leo, Sept 21, 2025 kwenye Mkutano wa kutambulisha Wagombea wa nafasi za Udiwani uliofanyika katika uwanja wa Salunda Shule ya msingi na kusisitiza kuwa Dk. Samia hataki maneno bali ni Kiongozi wa Vitendo.


Amesema kuwa, wakazi wa Mji wa Bariadi wanahitaji kiongozi atakayetembea na shida za Wananchi ambaye ni Dk. Samia Suluhu Hassan ambapo katika ziara yake mjini Bariadi hivi karibuni, aliahidi ujenzi wa soko na tayari fedha zimetolewa na limeanza kujengwa.


"Tunaanza safari mpya yenye Ilani ya 2025/2030, inasema kuchochea Mapinduzi ya kiuchumi wa kisasa, fungamanishi, rahisi unaojumuisha Watanzania wote... Uchumi wa kisasa huwezi kuiacha Teknolojia, Kilimo, Barabara, Umeme, mawasiliano, Maji na bima kwa wote, hiyo ndio Ilani inayokwenda kubadilisha maisha na Wana Bariadi" amesema.


Ameeleza kuwa kwa niaba ya wananchi wa Bariadi, endapo atachaguliwa atabeba mahitaji ya wananchi kumpelekea Rais Dk. Samia ili aweze kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maendeleo Bariadi mjini.


Ameongeza kuwa Jimbo la Bariadi Mjini lenye kata 10, Madiwani wake watakusanya changamoto na matamanio ya kila kata kumpelekea Mbunge wao (Mhandisi Kundo) atakayeyapeleka kwa Rais Dk. Samia.


Awali, Mgeni Rasmi katika Mkutano huo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Joshua Mirumbe amewataka wananchi kuchagua Rais Dk. Samia ambaye ameendelea kuimarisha Uchumi wa Taifa. 


Amesema kuwa uimarishaji wa Uchumi umetafsiriwa katika Ilani ya CCM katika sekta ya Viwanda ili vijana na Wanawake waweze kupata ajira na kuongeza vipato. 


"Ilani ya Uchaguzi ya 2025/2030 imetoa kipaumbele kutoa ajira katika sekta z Elimu na Afya sababu shule, zanahati, vituo vya Afya na Hospitali zimejengwa ili kuhudumia wananchi" amesema.


Jimbo la Bariadi Mjini lina kata 10 ambazo ni Bunamhala, Isanga, Guduwi, Mhango, Nyakabindi, Bariadi, Sima, Malambo, Somanda na Guduwi.


Mwisho. 













Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI