Header Ads Widget

CHAMA KINACHOUNGA MKONO EU KINAKARIBIA KUSHINDA UCHAGUZI LICHA YA MADAI YA KUINGILIWA NA URUSI

 

Chama kinachounga mkono Ulaya cha Rais wa Moldova Maia Sandu kinaelekea kupata ushindi na wingi wa wabunge katika uchaguzi unaoonekana kuwa muhimu kwa mustakabali wa nchi yake kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Sandu alikuwa ameonya kuhusu "uingiliaji mkubwa wa Urusi" baada ya kupiga kura, akisema mustakabali wa nchi yake, inayozungukwa na Ukraine na Romania, uko hatarini.

Chama chake cha Action and Solidarity (PAS) tayari kilikuwa kimepata 50% ya kura, huku kura nyingi kati ya 1.6m zikiwa zimehesabiwa, kikiwa kifua mbele ya Muungano unaopendelea Urusi ulio chini ya 25%.

Waliojitokeza walikuwa 52%, idadi ya juu kuliko miaka ya hivi karibuni.

Mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani, Igor Dodon, alikuwa amedai ushindi hata kabla ya matokeo na akaitisha maandamano nje ya bunge siku ya Jumatatu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI