Header Ads Widget

CCM MOROGORO MJINI WAZINDUA KAMPENI


Na Matukio Daima Media Morogoro.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Abdulaziz Abood amewataka wananchi kuendelea kumuamini ili kukamilisha miradi aliyoianza, huku akiahidi kuimarisha sekta za kijamii na kiuchumi.

Dkt Abood ameahidi Neema ya maendeleo katika kipindi cha miaka mitano ijayo iwapo wananchi watamuamini na kumchagua tena Katika kuwawakilisha katika kipindi cha miaka mitano.

Aidha akamuombea kura Mgombea Urais wa chama hicho Mhe Samia Suluhu Hassan na kumpongeza kwa hatua kubwa ya kuleta Fedha nyingi Katika Jimbo hilo kwaajili ya Utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuwaomba Watanzania waendelee kumuamini sambamba na wagombea Udiwani wa chama hicho.

 Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Mhandisi Joseph Masunga amewataka wanachama na wafuasi kufanya kampeni za amani na kuepuka vitendo vya uchochezi.


“Hakuna sababu ya kugombana kwa ajili ya siasa, tuendelee kushirikiana kwa amani ili chama kishinde kwa hoja na mshikamano,” alisema Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa na kuhimiza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika miaka mitano iliyopita  ni ushahidi tosha kuwa Serikali ya CCM inatenda kwa vitendo.



Viongozi hao wameeleza kuwa umoja na mshikamano wa wanachama ndio utakaohakikisha ushindi wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu ujao.


Baadhi ya wananchi walimuomba Mhe Abood pindi akichaguliwa tena Katika nafasi ya Ubunge aweke kipaumbele kwenye utatuzi wa changamoto za maji na Miundo mbinu ya barabara.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI