Header Ads Widget

TANZANIA NA ALGERIA KUSHIRIKIANA KATIKA UPATIKANI WA DAWA SALAMA,BORA NA FANISI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), Dkt. Adam Fimbo akisalimiana na Waziri wa Dawa nchini Algeria  


Tanzania na Algeria zimekubaliana kushirikiana katika kuboresha uhusiano kwenye upatikanaji na uzalishaji wa dawa zenye usalama, ubora na ufanisi  katika nchi hizo. 

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Dawa nchini Algeria  alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Wizara ya Afya Tanzania ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), Dkt. Adam Fimbo pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Iman Njalikai wakati wa ziara ya kiudhibiti iliyofanyika sambamba na  maonesho ya biashara ya kimataifa (IATF, 2025).

Katika ziara hiyo iliyolenga kuimarisha mahusiano na kubadilishana uzoefu na kuhamasisha uwekezaji katika eneo la dawa ilihusisha maafisa weilngine kutoka Wizara ya Afya na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).



Jumla ya viwanda vikubwa saba (7) vilitembelewa ikiwemo kiwanda cha Saidal kinachomilikiwa na Serikali ya Algeria, kiwanda cha Sophal, Orion Laboratories, Biopham, Biocare na Frater Raizers.

Viwanda hivi vimeonesha nia ya kuwekeza Tanzania kwa kuanza na uuzaji wa bidhaa ambazo ni haba na zenye uhitaji mkubwa ikiwemo dawa za matibabu ya saratani. Aidha viwanda hivi vimeahidi kuanzisha viwanda vya dawa nchini Tanzania hatua itakoyasaidia kupunguza gharama za upatikanaji wa dawa na utegemezi katika kuagiza dawa nje ya nchi.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI