Header Ads Widget

ALLY HAPI AZINDUA KAMPENI ZA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI

Katibu Mkuu Wazazi Ally Hapi akimnadi mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni Mhe Abbas Tarimba leo Septemba 13,2025 katika viwanja vya Mwinjuma Kinondoni.


KATIBU Mkuu Wazazi, Ally Hapi (MNEC) leo Septemba 13, 2025 amezindua rasmi kampeni za Ubunge Jimbo la Kinondoni zilizofanyika uwanja wa Mwinjuma Kata ya Kinondoni Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Ally Hapi  amewashukuru Wanançhi Kinondoni kwa kujitokeza kwa wingi ambapo amewahakikishia kuwa wamepata mtu sahihi na mchapakazi, mnyenyekevu, anajishusha kwa watu wote wa juu na chini huku akiwataka kutokuwa na mashaka nae.

"Nimewahi fanya kazi hapa Kinondoni kama Mkuu wa Wilaya, nafahamu uwezo wa Mgombea wetu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Kinondoni Mheshimiwa Tarimba na sina shaka nae kabisa mpeni kura nyingi za Ndiyo Oktoba 29 na pia kwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan na Madiwani wote kutoka CCM.




Tuvunje makundi, na sasa tukunjue mioyo tutafute kura kwa Mbunge, Rais na Diwani Chama kinataka Mafiga matatu.

"Tarimba anatosha, aliyepewa kapewa,  Alieandikiwa kwa wakati wake ni Ndugu Tarimba, tumuunge mkono, wale wenye vifundo vya hapa na pale fungueni mioyo, Chama kimeshamaliza uteuzi, na hakuna uteuzi mwingine.

Ninayemnadi namjua tokea nikiwa Mkuu wa Wilaya hapa Kinondoni, Kwa sasa mizengwe tupa pembeni tusonge mbele," Amesema Ally Hapi.



Na kuongeza kuwa: "Ambaye anawaza ndoto za uteuzi anaota ndoto za abunuwasi.

Watu wangu wapo 'field' najua kinachoendelea Kinondoni, Tarimba apewe ushirikiano na wale marafiki zangu waliogombea na Tarimba, tunawapenda na tuna waheshimu lakini tunawakumbusha Chama kwanza, mtu baadae.

Ndugu yangu Nyamwija, Iddi Azan hawa hawana tatizo... tuungane najua hamna tatizo, Shida ipo kwa wapambe. 

Ally Hapi akiwanadi Wagombea Udiwani wa Kata  za Jimbo la Kinondoni 




Wapambe wanaweza kulia sana kwenye msiba kuliko mwenye msiba mwenyewe, wapambe nuksi. Wapambe fungueni mioyo, tunajua wapo wapambe wa chini, katikati na wa juu pale.

Tumuunge mkono ndugu yetu Tarimba...Anatosha, ana sifa, ana uwezo na Chama kimemuamini, kila jambo lina wakati wake" Amesema Ally Hapi.

Aidha, amemuombea kura za kishindo mgombea Urais wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan kwani ndiyo kiongozi shupavu ambaye aliipokea nchi katika wakati mgumu na na ameweza kitimiza malengo ya awali na sasa anaenda kukamilisha zaidi.

"Oktoba tunatiki kura za kutosha kwa Samia, sote tutakumbuka, ametuvusha katika kipindi kigumu cha COVID 19, na hii anapaswa kutunukiwa nishani iliyotukuka, miradi yote mikubwa ameendelea nayo na inaenda vizuri na anaomba kura zenu kwa wingi ilikuendelea kukamilisha kazi iliyoianza." Amesema Ally Hapi.

Abbas Tarimba akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za Jimbo la Kinondoni leo Septemba 13,2025

Baadhi ya Wananchi na Wana CCM ka to ila tukio hilo 


Kwa upande wake mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni Mhe Abbas Tarimba amewashukuru Wananchi kujitokeza kwa wingi na kwamba ana deni kubwa kwao.

"Mwitikio huu ni dhahiri nina deni kubwa sana kwenu.

Kinondoni inaenda kuwa kama Masaki na shule na Miundombinu bora. Ikifika Oktoba 29 kwenye karatasi ya kupiga kura, jina langu ni jina la TARIMBA, kwa maana hiyo nimekuja kwa unyenyekevu mkubwa, nimejawa ukarimu na upendo, nimejawa na huruma, ningependa mimi na nyie kwa upando wetu, tunatiki kura kwa Tarimba." Amesema Tarimba.

Aidha, kutokana na kasi kubwa ya maendeleo, hasa ujenzi mkubwa wa daraja la Jangwani na miradi mikubwa katika Kata za Jimbo hilo zikiwemo Magomeni, Mzimuni, Kigogo na Hananasifu amewataka Wananchi wenye nyumba wasiuze nyumba zao kwani maeneo mengi yanaenda kuwa makubwa na yenye uchumi.

Mhe. Tarimba pia amewaomba wana Kinondoni kuwachagua Madiwani wa Kata zote 10 za Jimbo hilo ili aweze kufanya nao kazi vyema kuleta maendeleo.


Kwa upande wake MNEC wa CCM , Richard Kasesela amewaomba Wananchi wa Kinondoni kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi CCM kwani hali iliyopo sasa na Maendeleo yanaletwa na Chama hicho hivyo ametumia wasaha huo kuwaomba Wanachama wa CCM na Wananchi kujitokeza siku ya kupiga kura na kukichagua kwa kishindo.

"Kura milioni 4.4 za Dar tulizopewa 'target' zitapatikana. 

Kosa kubwa ni usaliti, na tunaamini usaliti kwa sasa hakuna na tutafanikisha kupata kura milioni Nne (mil 4),

"Siku ya kupiga kura tutakaguana vidole, ukimuona mwana CCM kidole chake hakina rangi, ujue huyo ame tusaliti.

Kila mmoja atembee kidole juu na mwanaccm utamkagua na kama hana rangi ya kupiga kura hiyo Oktoba 29.

"Mpeni kura TARIMBA kwani hata siku ya Wananchi hakuvaa jezi na zaidi alivaa nyeupe na nyeusi ilikuwapenda pia na Wana Simba, hivyo kura zake mpeni,

Pia kura nyingi kwa Madiwani wote wa CCM na rais wetu Samia Suluhu Hassan." Amesema Kasesela



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI