Header Ads Widget

YERICKO NYERERE AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA BAADA YA KUJIUNGA CHAUMMA

 


MWANDISHI wa vitabu na mwanasiasa nchini, Yericko Yohanesy Msambila Mkana Nyerere aliyekuwa Mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na hivi karibuni kuachana na chama hicho na kwenda Chama kingine cha upinzani cha CHAUMMA, leo Agosti 9,2025 kupitia mitandao yake ya Kijamii amefunguka na kueleza:

"Baada ya kuachana na siasa za Chadema, Ninajisikia mwenye amani ya moyo sana, Ninajisikia mwepesi na mwenye furaha isiyokifani. Akili yangu imetulia sana, nimerejea kwenye utimamu wa mwili, akili na moyo. 

Hakika vita vya wenyewe kwa wenyewe ni vigumu sana. Poleni niliowaumiza, Nami ninawasamehe mlioniumiza.

Sasa Ninatangaza msamaha kwa wote walionitusi kila aina ya matusi kwa kipindi cha miezi 12 hivi tangu mchakato wa kampeni uchaguzi wa Chadema hadi juzi nilipohama Chadema nakujiunga na Chama halisi cha Kisiasa CHAUMMA 

 Ninawafungulia/unblock wote niliowablock kwasababu ya matusi yao kwangu katika mitandao yangu ya Twitter/X, Instagram, facebook, nk.

Ukurasa mpya wa siasa za mageuzi umefunguliwa, Lugha yetu mpya ya kisiasa imefunguliwa, Siasa za Hoja zimerejea, Lugha za shombo na matusi zimefungwa rasmi.

Karibuni marafiki, mashabiki na wafuasi wangu katika ulimwengu mpya wa mitandao ya kijamiii. 

Siasa zangu sasa zitahusu sera na misiamo ya Chaumma, Ilani ya Chaumma, mrengo wa Chaumma, Itikadi ya Chaumma. Lugha ya kisiasa kwa sasa itakuwa ya Chaumma.



Aidha, tayari Yericko Nyerere ametangaza kugombea Ubunge kupitia Jimbo la Kigamboni kwa Chama hicho cha CHAUMMA.

Yericko Nyerere ni Mkazi wa Kigamboni eneo la Mbutu Dar es salaam, Ni mzaliwa katika Kijiji cha Maduma, wilaya ya Mufindi, mkoa wa Iringa, Tanzania, 4 Aprili 1983, ambapo pia mbali ya Siasa anamiliki kampuni yake ya Yecco Group Limited.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI