Header Ads Widget

ASKARI WA UHIFADHI POLOLETI WATAKIWA KULINDA HADHI YA JESHI HILO

  


Na,Jusline Marco;Arusha

Kamishna wa uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro NCAA Abdul-razaq  Badru amewataka askari wa uhifadhi katika pori la akiba la Pololeti Wilayani Ngorongoro kuzingatia maadili,weledi na matokeo ya kazi wanazozifanya ili kulinda hadhi ya jeshi hilo.



Kamishna Badru ametoa wito huo wakati akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua hali ya uhifadhi na ilinzi katika eneo hilo na kuzungumza na baadhi ya askari hao.


Aidha ameonesha kuridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na askati hao hali iliyopelekea eneo hilo kuwa na idadi kubwa ya wanyama mbalimbali wakiwemo tembo, swala, twiga, pofu, nyumbu na pundamilia.



Ameongeza kwa  kuwahakikishia askari hao kuwa miundombinu mbalimbali ya eneo hilo itaboreshwa sambamba na kujengwa kwa mazingira bora ya kufanyia kazi ili kuendelea kuboresha mazingira ya ulinzi na uhifadhi endelevu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI