KWA WANA-ISIMANI, WANA-IRINGA NA WATANZANIA WENZANGU!
Napenda kuchukua fursa hii kujulisha wanaCCM Wananchi wote wa Isimani kuwa jimbo la Isimani tumeshapata Mgombea nafasi ya Ubunge ambaye ni Mh Wiliam Vangimembe Lukuvi naomba niwajulishe kuwa tayari nimeshamtumia meseji Mh Lukuvi kumpongeza kwa ushindi na uteuzi wa kulitetea jimbo la Isimani pia nitaongea na vyombo vya habari kutoa hotuba ya kumuunga mkono Mh Lukuvi ili tupate ushindi wa Kishindo katika chama chetu CCM kwanza kwa Mh Rais wetu Dr Samia Suruhu Hassan, Mbunge wetu Mh Wiliam Lukuvi na Wah Madiwani wote 13 katika jimbo la Isimani!
KAZI NA UTU TUNASONGE MBELE.
Mimi Festo Shemu Kiswaga 24/8/2025
Mtia CCM nia Jimbo la Isimani 2025
0 Comments