Na,Jusline Marco;Dar es Salaam
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana ameipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro NCAA kwa kuvuka lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 269.9 kutoka lengo la shilingi bilioni 230.
Dkt.Chana ametoa pongezi hizo katika uzinduzi wa siku maalum ya Ngorongoro iliyopewa jina la Ngorongoro Day ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya maonesho ya 49 ya biashara ya kimataifa Sabasaba.
Aidha amemuelekeza Meneja wa Huduma za Utalii na Masoko Bi. Mariam Kobelo katika siku hiyo ya Ngorongoro kutangaza utalii kwa nguvu zote ili kupata wageni wengi zaidi.
Ameongeza pia kwa kuwapongeza watendaji wa wizara hiyo kwa kutimiza malengo ya ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kufikisha idadi ya watalii milioni tano kama ilivyoainishwa kwenye ilanı ya chama hicho.
“Niwapongeze sana watendaji wenzangu wa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na wadau wa sekta ya utalii kwani ilanı ya CCM ilitutaka tufikishe watalii milioni tano na sasa tunatembea kifua mbele kwani idadi hiyo imetimia.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Ephraim Mafuru amesema bodi hiyo kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na utalii zitaendelea kushirikiana ili kuhakikisha kuwa idadi ya watalii na mapato ya serikali kupitia sekta hiyo yanaongezeka.
0 Comments