Header Ads Widget

MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA DARASA LA SABA 2021,SOUTHERN HIGHLAND YAONGOZA KIWILAYA

Uongozi wa shule ya Southern Highland iliyopo Mafinga Mkoani Iringa unawapongeza wanafunzi wake wote waliofanya mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka 2021 kwa kufaulu vizuri mtihani huo na kuendelea kuipa heshima iliyotukuka shule hiyo na imekuwa ya kwanza kiwilaya kwa mara nyingine tena.

kutokana na matokeo yaliyotangazwa leo, Shule ya Southern Highland imekuwa ya kwanza kiwilaya  kati ya shule 12 na ya 4 kimkoa kati ya shule 146 huku Kitaifa ikishika nafasi ya 144 kati ya shule 5664

Uongozi wa shule ulisema wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba walikuwa 32 huku wastani wa shule ni 246.8438 na kundi lake ni chini ya wanafunzi 40

Na katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo tarehe 30 Oktoba shule ya Southern jumla ya wanafunzi 21 wamefaulu kwa alama A huku wanafunzi 11 wamefaulu kwa alama B na hakuna mwanafunzi aliyepata C, D na E. 

Hivyo Uongozi unapenda kutoa shukrani na pongezi kwa wazazi pamoja na walezi kwa kuchagua  Southern highland kuwa shule bora kwa watoto wao na pia wamewakaribisha wazazi wengine wawalete watoto wao katika shule hiyo ili wapate elimu bora na malezi mazuri.

Uongozi wa shule unatangaza  nafasi za masomo kwa mwaka 2022 kuanzia darasa la awali hadi darasa la saba pia tunakaribisha wote wanaohitaji kuhamishia watoto wao kuja kusoma Southern Highlands Mafinga  nafasi zipo piga simu 0752840884/0754651966



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI