Na Fatma Ally Matukio DaimaApp
Tanzania inatarajia kuwa mwenyejeji wa Tuzo za 32 za kimataifa za utalii" World Travel " ukanda wa Afrika na Bara la Hindi zitakazotolewa Juni 28 Jijini Dar es salaam chini ya uratibu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) .
Aidha, heshima hii ya kuwa mwenyeji wa tuzo hizi ni matokeo ya jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake wa kutangaza sekta ya utalii.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru amesema Tanzania imepata heshima kubwa huku wageni 500 wakitarajiwa kushiriki.
Amesema kuwa, lengo la Tuzo hizo ni kuwatambua wadau mbalimbali wakiwemo mashirika ya ndege, watoa huduma za malazi, vivutio vya utalii, wakala wa biashara za utalii, vivutio vya utaliii, mamlaka za usimamizi na utangazaji wa utaliima wadau wengine na zimekuwa chachu ya ubunifu, ushindani na kuboresha viwango vya huduma.
Ameongeza kuwa, kwa upande wa Tanzania kuna wadau 38 kutoka sekta binafsi na 12 kutoka Serikalini ambao wanawania Tuzo hizo.
Ameongeza kuwa, Tuzo hizo zimeandaliwa na Kampuni ya World Laxuary media Group ambapo zitatolewa Juni 28 mwaka huu katika Hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es salaam .
"Tuzo hizi ziliazishwa mwaka 1993 na zinalengo la kutambua, kuthamini na kusherehekea mchango wa wadau katika sekta ya Utalii na Ukarimu duniani, ambapo kuna Tuzo mbalimbali za utalii hizi ndizo Tuzo kubwa za utalii katika dunia na zinafanyika kwa Kanda"amesema
Aidha amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo amekuwa akiifanya ya kutagaza utalii na kuridhia kuwekeza katika sekta utalii.
"Rais Dkt Samia amekuwa mstari wa mbele kuingia na kuwekeza na kuutagaza Tanzania kupitia filamu ya The Royal tour."alisema
Katika hatua nyingine Mafuru alitoa wito kwa wadau mbalimbali katika sekta ya utalii kuchagamkia fursa hiyo .
Naye, Meneja Masoko wa Hospitali ya Shifaa Van Afrika ambao pia ni wadau washiriki katika Tuzo hizo, Victoria Tarimo, amesema hospitali hiyo itahakikisha wageni wote wanashiriki katika hafla hiyo wanapata huduma bora za afya zenye viwango.
Amesema hospitali hiyo imekua ikitoa huduma mbalimbali za afya hivyo kupitia hafla hiyo wanakwenda kumuunga mkono Rais Dkt Samia katika utalii tiba .
Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Hoteli ya Johari Rotana, Ahmed Said ambae ni miongoni mwa wadau washiriki katika Tuzo hizo, amesema wamejipanga kutoa huduma zenye viwango vya kimataifa katika hafla hiyo.
0 Comments