Header Ads Widget

SERIKALI KUENDELEA KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MIFUGO

 



Na Hamida Ramadhan, MatukioDaima App Dodoma


SERIKALI imesema imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kukabiliana na magonjwa ya mifugo ikiwemo kuhamasisha uogeshaji wa mifugo kwa kutumia dawa za kuua wadudu kama kupe pamoja na utoaji wa chanjo kwa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo. 


Hayo yamesemwa leo Juni 11,2025 jijini Dodoma na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Dkt.Ashatu Kijaji wakati aliwa pokuwa akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akiekeza kuhusu uzinduzi wa kampeni ya chanjo na utambuzi wa mifugo kitaifa utakaofanyika Juni 16,2025 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.


Amesema uzinduzi wa Kampeni hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuhakikisha inaboresha afya ya mifugo hapa nchini.


Amesema kwasasa Tanzania inakadiriwa kuwa na ng’ombe milioni 39.2, mbuzi milioni 28.6, kondoo milioni 9.7, kuku milioni 108.2 na nguruwe milioni 4.1. Pamoja na idadi hiyo ya mifugo bado mchango wa sekta hiyo kwenye pato la taifa mpaka sasa ni 6.2% huku akisema kuwa Mchango huu ni mdogo ukilinganisha na idadi ya mifugo tuliyo nayo.


Aidha Dkt.Kijaji amesema kuwa uwepo wa magonjwa mbalimbali ya wanyama ambayo huathiri uzalishaji wa mifugo kwa kusababisha vifo vya mifugo na kukosekana kwa ithibati ya kuuza mifugo na mazao yake katika masoko ya kimataifa ni miongoni mwa sababu inayopelekea mchango wa sekta ya mifugo kuwa mdogo kwenye pato la Taifa.


Hata hivyo,amesema serikali itatekeleza mpango wa chanjo kwa miaka mitano mfululizo kuanzia mwaka 2025 hadi 2029 kwa gharama ya shilingi bilioni 216.


Amesema awamu ya kwanza ya mpango huo jumla ya ng’ombe 19,097,223 watachanjwa dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Mapafu ya ngo’mbe (CBPP)


Pia mbuzi na kondoo 17,000,000 watachanjwa dhidi ya ugonjwa wa Sotoka ya Mbuzi na Kondoo (PPR) na kuku wa asili 40,000,000 watachanjwa dhidi ya mdondo wa kuku (ND), Ndui ya kuku na Mafua ya kuku.


Tukio la Uzinduzi wa kampeni ya Chanjo na utambuzi wa mifugo nchini litatanguiliwa na Kongamano la Wafugaji Tanzania lililoandaliwa na Chama cha Wafugaji Tanzania ambalo litafanyika Juni 14 – 15 2025 mjini Bariadi, Simiyu ambapo Mgeni Rasmi anataraniwa kuwa Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi CCM Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.


Hata hivyo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hiyo.



Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI