Na. Mwandishi Wetu, Kigamboni.
SERIKALI ya Mtaa wa Mbwamaji Gezaulole Kata ya Somangila Wilaya ya Kigamboni imewezesha Mafunzo ya Ujasiriamali kwa Wananchi wake ili kujikwamua kiuchumi sambamba na kuleta maendeleo.
Mafunzo hayo yanaratibiwa na Ofisi ya Serikali ya Mtaa huo kupitia kwa Mwenyekiti wake Mhe. Yohana Luhemeja Kashindye (Maziku) ambapo yanatolewa na Wawezeshaji kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu wazima nchini (TEWW).
Awali Mwenyekiti wa Mtaa huo, Mhe. Maziku amesema kama Mtaa wanaendelea kufanya juhudi mbali mbali za kuwainua Wananchi kiuchumi ikiwemo mafunzo hayo ya Ujasiriamali.
"Serikali ya Mtaa Mbwamaji tunamipango ya kiuwezeshaji kiuchumi kwa vikundi vya Wajasiriamali na Wananchi.
Kwa juhudi nikiwa kama Mwenyekiti tumeanza na mafunzo haya kwa sasa ni zaidi ya mwezi mmoja lengo na yataenda kwa miezi mitatu katika kuwasaidia Vijana wa Kike na wamama wawe na mafunzo ya Ujasiliamali wa kutengeneza vitu vya kujipatia vipato". Amesema Mhe Maziku.
Aidha, Mhe. Maziku ametoa wito na kuomba viongozi na wananchi kujitokeza kusaidia kwa kuwapa ujuzi na maarifa ya kujikwamua kiuchumi.
"Kwenye Mtaa wetu tuna vikundi vya Ujasiriamali, ikiwemo cha akina Mama lakini wanaupungufu wa vifaa ambavyo vinagharama ya Tsh.milioni 4.6.
Lakini pia bado tunahamasisha wanawake wote kushiriki mafunzo haya kila yanapotolewa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mafunzo hayo, Batuli Abilahi amemshukuru Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbwamaji kwa kuwawezesha mafunzo hayo ambayo yanaenda kuwajengea uwezo wa kiuchumi
Mafunzo hayo yanatolewa na Wawezeshaji kutoka IEA, akiwemo Bazila Mramba,
Atupele Shome na
Zenais Lymo huku wakifundisha masuala ya upisi wa keki, Upambaji wa keki, karanga za mayai, Utengenezaji wa sabuni ya maji.
Pia mafunzo ya utengenezaji wa sabuni ya magadi, Utengenezaji wa jiki, Utengenezaji wa dawa ya kusafishia talazo (tiles) na sink, Utengenezaji wa mazulia, Utengenezaji wa batiki,
Pia mafunzo ambavyo bado wanatarajiwa kupatiwa awamu inayofuata ni: mafunzo ya kutengeneza Mafuta ya kujipaka, Kupamba keki kwa fondant, Kuchovya batiki kwa rangi mbali mbali, Upishi wa vitafunwa mbalimbali kwa kutumia unga wa ngano, Utengenezaji wa Bustani na Ususi.
0 Comments