Header Ads Widget

IRAN YAWAKAMATA NA KUWANYONGWA WASHUKIWA KUFUATIA MZOZO WA ISRAEL

 Mamlaka ya Iran imewakamata na kuwanyonga watu kadhaa wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na mashirika ya kijasusi ya Israel, kutokana na vita vya hivi majuzi kati ya nchi hizo mbili.

Hatua hiyo inawadia baada ya kile maafisa wanaelezea kama kuingiliwa kwa huduma za usalama wa Iran na maajenti wa Israel.

Mamlaka zinashuku habari zilizotolewa kwa Israel zilihusika katika msururu wa mauaji ya hali ya juu wakati wa mzozo huo.

Haya yalijumuisha mauaji yaliyolengwa ya makamanda wakuu kutoka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na wanasayansi wa nyuklia, ambayo Iran inayataja kuwa yanahusishwa na watendaji wa shirika la kijasusi la Israel la Mossad wanaofanya kazi ndani ya nchi.

Wakitikiswa na ukubwa na usahihi wa mauaji haya, mamlaka zimekuwa zikimlenga mtu yeyote anayeshukiwa kufanya kazi na ujasusi wa kigeni, ikisema ni kwa ajili ya usalama wa taifa.

Wakati wa mzozo huo wa siku 12, viongozi wa Iran waliwanyonga watu watatu waliotuhumiwa kuifanyia Israel ujasusi.

Siku ya Jumatano - siku moja tu baada ya kusitishwa kwa mapigano - watu watatu zaidi walinyongwa kwa mashtaka sawa.

Maafisa wametangaza kukamatwa kwa mamia ya washukiwa kote nchini kwa tuhuma za ujasusi.

Televisheni ya taifa imerusha hewani madai ya kukiri makosa kwa wafungwa kadhaa, wakikubali kushirikiana na ujasusi wa Israel.

Mashirika ya haki za binadamu na wanaharakati wameelezea hofu yao juu ya matukio ya hivi punde, wakitaja mazoea ya muda mrefu ya Iran ya kulazimisha na kuendesha kesi zisizo za haki.

Kuna wasiwasi kwamba unyongaji zaidi unaweza kufuata. Wizara ya Ujasusi ya Iran inadai kuwa iko katika "vita visivyoisha" dhidi ya kile inachokiita mitandao ya kijasusi ya Magharibi na Israel - ikiwa ni pamoja na CIA, Mossad, na MI6.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI