Header Ads Widget

'IRAN ITAJIBU MAPIGO TENA IKISHAMBULIWA'- AYATOLLAH

Iran itajibu mashambulizi yoyote ya siku za usoni ya Marekani kwa kushambulia kambi za kijeshi za nchi hiyo Mashariki ya Kati, Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei alisema Alhamisi, katika hotuba yake ya kwanza kwenye televisheni tangu kufikiwa kwa usitishaji vita kati ya Iran na Israel.

"Jamhuri ya Kiislamu iliishangaza Marekani peupe. Ilishambulia moja ya kambi muhimu za Marekani katika kanda," Khamenei alisema.

Khamenei alisisitiza kuwa Marekani "haijapata mafanikio yoyote" kutokana na mashambulizi yake dhidi ya vituo vya Iran vya nyuklia.

Ayatollah Ali Khamenei alisema mashambulizi hayo "hayakufanikisha lolote la maana" kutatiza mpango wa nyuklia wa Iran, na alielezea kulipiza kisasi dhidi ya kituo cha anga cha Marekani huko Qatar kama "pigo kubwa".

Iran haitajisalimisha

Katika hotuba zake zilizorekodiwa awali, zilizosambazwa kwenye televisheni ya serikali, Khamenei aliahidi kwamba Iran haitajisalimisha licha ya wito wa Marekani.

"Rais wa Marekani Donald Trump aliweka wazi kuwa Wamarekani hawatataka kingine chochote zaidi ya kujisalimisha... tukio kama hilo halitatokea kamwe, "Khamenei alisema.

Alipoulizwa ikiwa Marekani itashambulia tena Iran ikiendeleza mpango wake wa kurutubisha nyuklia, Trump alijibu "ndio".

Wakati huo huo, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth amesema taarifa za kijasusi zilizokusanywa na Marekani na Israel zilionyesha kuwa operesheni hiyo "iliharibu mpango wa nyuklia kwa kiasi kikubwa, na kuurudisha nyuma kwa miaka".

Tehran kwa miongo kadhaa imekuwa ikikanusha shutuma za viongozi wa Magharibi kwamba inatafuta silaha za nyuklia.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI