Na Fatma Ally Matukio DaimaApp
Aliyekua Mwenyekiti wa Uvccm Vyuo na Vyuo vikuu mkoa wa Dodoma Salum Ismail amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi Octoba kupiga kura katika uchaguzi mkuu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini amesema kuwa, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan ameweka mazingira rafiki kwa vijana kuweza kugombea .
Amesema kuwa, aametia nia kugombea Ubunge Jimbo la Kahama mjini mkoani Shinyanga.
Amesema kuwa lengo la nia ya kugombea ni Kwa ajili ya kuwaketea maendeleo Wananchi wa Kibaha mjini kwani kupitia fursa nyingi zilizopo jimboni huko ikiwemo migodi ya Madini.
Katika hatua nyingine Salum amekemea wanasiasa na wanaharakati wanaochochea uvunjifu wa Amani Nchini hivyo amesema kuwa watahakikisha wanapambana nao.
Aidha ametoa wito kwa Watanzania kumuunga mkono Rais Samia kutokana na mazuri aliyoyafanya.
Kwamba Wakati anapokea kijiti Cha uongozi baada ya kifo cha Rais Dkt. John Magufuli kulikuwa na miradi mingi ambayo ilikuwa ikiendelea.
Amesema kuwa kutokana na Mazingira hayo watu wengi walidhani Rais Samia asingeweza kuiendeleaa na kuikamilisha, hata hivyo ameitekeleza vizuri na kuikamilisha jambo ambalo linafanya Watanzania wamuunge mkono.
Amekemea watu wanaomkejeli na kumsema vibaya kwamba hawatawavumilia.
Nimedhamkria na nmetia Nia ya kugombea Jimbo la kahama mjini.
Nimefikiria kuwa naweza kuwasaidia wananchi katika kuyaendea maendeleo.
Aidha, amesema Rais Samia amepita katika mapito mengi lakini amehakikisha hali ya usalama wa Nchi inakuwa vizuri.
"Sisi kama makanda na vijana wasomi na watanzania atupo tayari kuona RAIS anabezwa kwa vyovyote vile, hatupo tayari kuona mtu mwenye viashiria vya uvunjivu wa amani katika nchi ya Tanzania".
Aidha, miradi yote ya kimkakati imetekelezwa na imekamilika,tatizo la umeme, miundombinu ya barabara imetanuliwa.
0 Comments