Header Ads Widget

MSIMU WA TATU WA MBIO ZA KIMATAIFA ZA SWAHILI ZIMEZINDULIWA RASMI JUNI 25 JIJINI ARUSHA.

 


Na,Jusline Marco;Arusha

Zaìdi ya washiriki 800 wanatarajiwa kushiriki mbio za masafa za kimataifa za Swahili Tanzania msimu wa Tatu zinazotarajiwa kuanza Juni 28 mwaka huu jijini Arusha zenye lengo la kuthamini sekta ya michezo katika kukuza na kuendeleza lugha adhimu ya kiawahili.

Akizungumza katika uzinduzi wa mbio hizo leo juni 24,2025 Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Utamaduni Boniface Kadili amesema mbali na lengo hilo pia zimelenga kutangaza utalii wa ndani wa utamaduni na utalii wa asili,utalii wa mbuga pamoja na kuvitangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini hususani katika mkoa wa Arusha sambamba na kuhamasisha umuhimu wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya ya akili.

Aidha amesema kuwa katika kuelekea kuadhimisha siku ya kiswahili Duniani ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Julai 7, nchi zilizoendelea na nchi za Afrika huungana kuadhimisha siku hiyo na kuipa umuhimu ambapo amesema kauli mbiu ya mwaka huu kwenye mbio hizo isemayo "Kiswahili kwa Amani na mshikamano" ndiyo itakayo tumika katika maadhimisho hayo.

"Niwafahamishe wananchi wa makundi mbalimbali kushiriki mbio hizi ikiwa mi kuunga mkono juhudi za kukuza,kuendeleza lugha ya kiswahili kupitia michezo."


Kwa upande wake Mkurugemzi Mtendaji wa African Sports Agency Bwn.Joseph Msele amesema kuwa kama taasisi itafanya kila linalowezekana kuhakikisha kila mtu afahamu kuwa lugha ya kiswahili kuwa kimezaliwa Tanzania kwa kushirikiana na Bakita ni kuanzisha mbio hizo.

Amesema kupitia mbio hizo wanazo ndoto za kuzifanya ziwe mbio kubwa duniani huku ikifika mwaka 2040 ziwe miongoni mwa mbio kumi bora duniani ambapo amewaomba wadau wenye nia njema kuungana kwa pamoja kushiriki kikamilifu ili kuionyesha dunia vile ambavyo lugha hiyo inaenziwa ili kufikia malengo hayo.


Ameongeza kuwa mbio hizo za kitanzania na itakuwa ndiyo utamaduni wa watanzania kuweza kufanya mazoezi kwa afya pamoja na kudumisha lugha ya kiswahili kama utamaduni ambapo ameshauri mbio hizo zisambae katika mikoa yote huku Mkoa wa Arusha ukiwa ndiyo Mkoa mama wa mbio hizo.

Awali Katibu Mtendaji kutoka Bakita Bi.Consolata Mushi amesema maadhimisho ya siku ya kiswahili duniani kufanyika Julai 7 ni itatoa fursa kwa watanzania wote kuenzi siku hiyo ambapo mbio hizo ni maalum kwa ajili ya kuienzi lugha hiyo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI