NA FRANCIS GODWIN ,MATUKIO DAIMA
Takribani watu milioni Ishirini wanafariki kwa mwaka mmoja kutokana na magonjwa ya moyo yanayosbabishwa na kukaa kwa muda mrefu bila ya kusimama.
Maisha ya maelfu ya watu yanaweza kuokolewa ikiwa watu wangejua jinsi ya kugundua dalili za mapema za mshtuko wa moyo.
Akizungumza katika kipindi cha Asubuhi ya Moto kilichorushwa na Matukio Daima Media jana Mkurugenzi wa Hopsitali ya Heameda Dkt Herry Mwandolela ambaye pia ni Daktari wa Magonjwa ya moyo amesema kuwa kutokana na takwimu za mwaka Jana zinaonesha kuwa watu wengi wanakufa kutokana na ugonjwa wa moyo unaosababishwa na kukaa kwa muda mrefu bila ya kusimama.
Dkt Mwandolela
"Kwa takwimu za mwaka Jana zinaonesha takribani watu milioni Ishiri wanafariki ndani ya mwaka mmoja kwa ugonjwa wa moyo ambao unatokana na kukaa kwa muda mrefu bila ya kusimama".
"Pia vipo viashiria vingi ambavyo mtu akiwa anakaa kwa muda mrefu bila ya kusimama atapata ugonjwa wa moyo japo kuwa anaweza akapata na magonjwa mengine Kama vile kisukari, na saratani.
Hivyo anapaswa kujua changamoto haiji kwa haraka huwa inakuja taratibu Sana na inaweza kumpata mtu miaka kadhaa mbele".
Caedmon Mtweve amesema kuwa ugonjwa wa moyo hautokani na kukaa kwa muda mrefu tu ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi vinaweza kusababisha ugonjwa wa moyo.
"Ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi vinaweza kuathiri moyo kwasababu mafuta yanaenda kuganda kwenye mishipa ya damu na kusababisha damu kutokufanya kazi vizuri".
Hivyo kutokana na kuendelea kwa magonjwa ya moyo hatuna budi kutafuta nafasi ya kufanya mazoezi walau Kila siku japo dakika chahe ili tuweze kuepuka ugonjwa huo wa moyo hasa wafanyakazi wa maofisini na madreva wa magari ya abiria na mizigo.
Sera ya afya inalenga kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kama magonjwa ya moyo kwa kusisitiza elimu ya afya ,kinga na upatikanaji wa matibabu stahiki .
Hata hivyo kwa muda sasa Serikali imeendelea kutoa kipaumbele katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya zenye ubora na zinazowafikia wananchi wote ili kuboresha afya zao.
Serikali inatambua kuwa afya bora ni rasilimali muhimu kwa maendeleo ya taifa, kwani maendeleo ya Tanzania yanategemea wananchi wenye afya njema na uwezo wa kuzalisha mali.
Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya, Serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika utoaji wa huduma hizo kwa kuzingatia sera na miongozo iliyopo.
mfano sera ya afya iliyosainiwa na aliyekuwa waziri wa afya David Mwakyusa Juni 2007 ni sera iliyokuwa ikiongoza utoaji wa huduma za afya ilipitishwa mwaka 1990.
Tangu kupitishwa kwake, kumekuwepo na mabadiliko mbalimbali ya kiuchumi na kijamii, maendeleo ya sayansi na teknolojia, pamoja na kuongezeka kwa magonjwa. Aidha, Serikali imetoa maelekezo mbalimbali ambayo yameleta changamoto mpya katika utoaji wa huduma za afya.
Mabadiliko haya kwa pamoja yameifanya Sera ya Afya ya mwaka 1990 kutokidhi kikamilifu mahitaji na matarajio ya sasa na ya baadaye.
Vilevile, mfumo na utaratibu wa utoaji wa huduma za afya unaotumika kwa sasa umebadilika kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na ule uliokuwa ukiongozwa na sera hiyo.
Mwaka 1996, marekebisho ya sera yalifanyika kwa lengo la kuanzisha mfumo mpya wa utoaji na usimamizi wa huduma za afya katika ngazi ya wilaya.
Marekebisho hayo yalitambua na kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika utoaji wa huduma za afya.
Pia, yalihamishia baadhi ya majukumu ya usimamizi wa utekelezaji wa huduma za afya kwa mamlaka za Serikali za Mitaa, jambo lililoongeza ushiriki wa wananchi katika kusimamia na kumiliki rasilimali za afya.
Kutokana na mabadiliko hayo, ilibidi Sera ya Afya ya mwaka 1990 ifanyiwe mapitio kwa kuzingatia sera na mikakati mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
Miongoni mwa sera na mikakati hiyo ni Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Malengo ya Maendeleo ya Milenia, pamoja na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA).
Sera ya Afya ya mwaka 1990 iliyopitiwa mwaka 2007 imeweka wazi dira, malengo na maelekezo ya Serikali kuhusu utoaji wa huduma za afya. Aidha, imezingatia mabadiliko ya kiuchumi na kijamii, matokeo ya tafiti na majaribio mbalimbali, pamoja na uzoefu uliopatikana katika utoaji wa huduma za afya nchini.
Utayarishaji wa sera hii ulifanyika kwa njia shirikishi, ambapo Wizara iliwashirikisha wadau mbalimbali wanaotoa na kutumia huduma za afya katika mchakato wa kupitia sera ya mwaka 1990.
Hivyo, jukumu la wadau wote katika sekta ya afya ni kuisoma, kuielewa na kutafsiri matamko yaliyomo katika sera hii wakati wa kupanga, kutoa na kutathmini huduma za afya nchini
Hata hivyo kwa sasa sera ya afya imekuja na bima ya afya kwa wote mpango ambao hautamuacha mtu.







0 Comments