Mbunge wa Iringa mjini Jesca Msambatavangu kushoto akishuhudia zoezi la utiaji sahii mkataba wa ujenzi wa barabara ya lami Mkimbizi -Mtwivila leo
NA MATUKIO DAIMA MEDIA
kutatuliwa kwa kero kubwa ya barabara ya Mkimbizi -Mtwivila ni heshima kubwa kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, mbunge wa jimbo la Iringa mjini Jesca Msambatavangu na diwani Eliud Mvela kwa kuanza ujenzi wa barabara ya lami Mkimbizi -Mtwivila ambayo itakwenda kutekelezwa baada ya mkataba kusainiwa Rasmi leo Juni 25 jijini Dodoma
Mchakato wa ujenzi wa barabara hiyo ulikuwa ni kitanzi na ungepunguza kura za diwani ,mbunge na hata Rais ila kwa sasa kama ni mtego bado CCM imekwepa mtego hupo.
Mvela alisema ujenzi huo umefikia hatua muhimu baada ya kuthibitishwa kuwa mkandarasi umesaini rasmi leo jijini Dodoma, hatua inayotarajiwa kufungua rasmi kazi ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa miundombinu.
Akizungumza na Matukio Daima Media Mvela ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Uchumi na Afya, amesema kuwa ndani ya siku 21 mkandarasi atakuwa ameanza kazi katika eneo la mradi, ambao unatekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kwa kushirikisha halmashauri sita, ikiwemo ya Iringa..
Mvela ameongeza kuwa katika mchakato wa ujenzi wa barabara hiyo pongezi na shukrani basi zifike kwa Mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu, kwa mchango wake mkubwa katika kusaidia utekelezaji wa maendeleo katika kata hiyo, akisema mafanikio yaliyopatikana yamewezeshwa kwa kiasi kikubwa na uongozi wake bora na ushirikiano mzuri.
“Katika kata nyingi maendeleo yanachelewa kwa sababu baadhi ya viongozi hawasemi changamoto zilizopo na kuzifikisha sehemu husika ukizingatia katika awamu hii tunayobahati ya kuwa na Rais msikivu na mwenye nia ya kusaidia, lakini anahitaji kufahamishwa ambapo ukiomba lazima upewe na bahati nzuri katika kata yetu tunaye Mbunge mchapakazi na msikivu ambaye kila nilipowasiliana naye kuhusu changamoto za wananchi, alikuwa tayari kushughulikia na kufanyia kazi.
Aidha ameeleza kuwa Mbunge Msambatavangu ni kiongozi wa vitendo, anayepambana kimya kimya kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa wakati, ikiwemo mradi wa ujenzi wa barabara ya lami katika kata ya Mkimbizi, ambao kwa kiasi kikubwa ameuhusisha na juhudi za mbunge huyo.
“Mimi namshukuru sana Jesca. Watu wengi hupenda viongozi wanaopiga kelele, lakini yeye ni wa vitendo zaidi. Ukimweleza jambo analifuatilia hadi mwisho na kwa hili niseme tu tuwasifu watu wakiwa hai, na mimi nasema kwa dhati kwamba Jesca amehusika kwa kiasi kikubwa kuhakikisha kata hii inapata barabara ya lami lakini pia amesaidia maendeleo ya maeneo mengine”
Aidha, amesema kuwa mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika kata hiyo yametokana na mchango wa viongozi, mashirika na wananchi waliotoa ushirikiano wa dhati katika kusukuma mbele maendeleo ya Mkimbizi
0 Comments