Japan imemnyonga mtu aliyewaua watu tisa mwaka wa 2017, ikiwa ni mara ya kwanza tangu 2022 nchi hiyo kupitisha adhabu ya kifo.
Mauaji ya mfululizo ya Takahiro Shiraishi, aliyepewa jina la "muuaji wa Twitter", yaliishangaza nchi na kuzua mjadala kuhusu jinsi kujiua kulivyojadiliwa mtandaoni.
Shiraishi, aliyekuwa na umri wa miaka 30 wakati huo, aliwarubuni waathiriwa wake - wengi wao wakiwa wasichana wa umri wa kati ya miaka 15 na 26 - kwenye nyumba yake, kabla ya kuwanyonga na kuwakatakata.
Mauaji hayo yalijulikana mnamo Oktoba 2017, wakati polisi walipata sehemu za mwili katika jiji la Japan la Zama, karibu na Tokyo, walipokuwa wakimtafuta mmoja wa waathiriwa.
0 Comments