Header Ads Widget

WIZARA YA UJENZI YAOMBA KUIDHINISHIWA NA BUNGE BAJETI YA ZAIDI YA SHILINGI TRILION 2.2

Na Hamida Ramadhani  Matukio Daima Pp Dodoma

WIZARA ya Ujenzi imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi, 2,280,195,828,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. 

Akiwasilisha Bajeti ya wizara hiyokwa mwaka wa fedha 2025/26 leo Mei 5,2025 Bungeni Dodoma Waziri wa Ujenzi  Abdallah Ulega amesema Kati ya fedha hizo, Shilingi 90,468,270,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ya Wizara na Taasisi na Shilingi 2,189,727,558,000.00 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.

Amesema Bajeti ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inajumuisha fedha za ndani Shilingi 1,209,223,117,000.00 nafedha za nje ni Shilingi 980,504,441,000.00.

Ulega amesema  Fedha za ndani zinajumuisha Shilingi 688,756,470,000.00 kutoka Mfuko wa Barabara na Shilingi 520,466,647,000.00 ni fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali.

Aidha amesema  katika mwaka wa fedha 2025/26, Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) imeweka malengo ya kusajili Wahandisi 3,820, Mafundi Sanifu 500, Kampuni za Ushauri wa Kihandisi 18 na maabara

Vilevile,Waziri Ulega amesema Bodi imepanga kusimamia utekelezaji wa mpango wa mafunzo kwa vitendo kwa Wahandisi Wahitimu 4,657ambapo Wahandisi Wahitimu watakaokuwa wanaendelea na mafunzo ni 4,317 na Wahandisi wapya 1,200.

"Mheshimiwa Spika, Bodi vilevile imepanga kuendelea kufanya kaguzi za shughuli za kihandisi nchini ili kuhakikisha kuwa shughuli zote za kihandisi zinafanywa na wahandisi waliosajiliwa na kwa kufuata maadili ya utendaji kazi za kihandisi," Amesama Waziri Ulega .

Amesema Bodi pia itaendelea na jukumu lake la kutembelea na kukagua miradi yote ya ujenzi ya kimkakati pamoja na barabara za Halmashauri pamoja na kusimamia mafunzo ya kujiendeleza kitaaluma kwa wahandisi watalaam na washauri. 

Aidha, Bodi itaendeleza jitihada za kuwashawishiwahandisi wataalam ili waanzishe kampuni za ushauri wa kihandisi mikoani kwa lengo la kusogeza huduma hii karibu na watumiaji.Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB)

"Mheshimiwa Spika, vilevile, Bodi imepanga kuwajengea uwezo Wahitimu 313 wa fani hizo kupitia mpango maalumu wa Mafunzo kwa Vitendo kwa Wahitimu wa Vyuo Vikuu (Architectural and Quantity Surveying Internship Programme – AQIP)," Amesema . 

Aidha, katika kutekeleza programu za kujengea uwezo Wataalam wa fani za Ubunifu Majengo, Ukadiriaji Majenzi, Ubunifu wa Ndani ya Majengo, Ubunifu wa Mandhari ya Nje ya Majengo, Usanifu Teknolojia ya Majengo, Utathmini Majengo, Usimamizi Ujenzi na Usimamizi Miradi, Bodi imepanga kuendesha mitihani ya kitaalamu kwa Wahitimu 340 katika fani za Ubunifu majengo na Ukadiriaji majenzi. 

Amesema Bodi pia imepanga kutembelea Vyuo Vikuu 5 ili kuwahamasishakuanzisha fani za Ubunifu majengo na Ukadiriaji majenzi ili kukuza idadi ya Wataalam hawa nchini. 

Aidha, Bodi pia itafanya mikutano 5 na Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na kuendesha mashindano ya Insha kwa lengo la kuhamasisha Wanafunzi hao kusoma masomo ya Sayansi na hatimaye kusomea taaluma za Ubunifu Majengo, Ukadiriaji Majenzi na taaluma nyingine zinazoshabihiana nazo.

"Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2025/26, Bodi imepanga kusajili jumla ya Makandarasi wapya 1,600 na kukagua jumla ya miradi ya ujenzi 3,550.Aidha, Bodi itaendesha kozi za mafunzo sita (6) na mafunzo ya ushirikiano wa ubia (Joint Venture) katika kituo kimoja,"Amesema Waziri Huyo. 

Vilevile, amesema  Bodi imepanga kufanya mkutano mmoja (1) wa mashauriano na wadau wa sekta ya ujenzi.

Ameeleza Bodi pia itaendelea kuendesha Mfuko maalum wa kutoa dhamana ya kusaidia Makandarasi wa ndani (Contractor’s Assistance Fund – CAF) pamoja na kuendelea kuhamasisha Makandarasi wa ndani kujiunga pamoja ili kuomba zabuni kwa mfumo wa ubia.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI