Kaimu Meneja wa kanda ya Magharibi wa Benki ya NMB Gadiel Sawe katika picha tofauti akikabidhi kwa Naibu Waziri wa TAMISEMI Zainabu Katimba (kulia) vitanda vya kujifungulia wajawazito, vitanda vya kulalia wagonjwa na vitanda vya wanafunzi vilivyotolewa kwa halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji na halmashauri ya wilaya Kigoma

Naibu Waziri wa nchii ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Zainab Katimba akizungumza katika hafla ya Benki ya NMB kukabidhi misaada mbalimbali yenye thamani ya shilingi Milioni 42.4 kwa ajili ya utoaji huduma kwenye sekta za afya na elimu mkoani Kigoma.

Katibu Tawala wa mkoa Kigoma Hassan Rugwa akizungumza katika hafla ya NMB kukabidhi vifaa vya elimu na afya kwa halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya wilaya Kigoma
Na Fadhili Abdallah, Kigoma
BENKI ya NMB imekabidhi misaada yenye thamani ya shilingi milioni 42.4 kwa ajili ya kusaidia upungufu kwenye sekta ya elimu na afya mkoani Kigoma ikiwemo kukabidhi vitanda 10 vya kujifungulia mama wajawazito kwa vituo vitano vya utoaji huduma ya afya vinavyotoa huduma ya mama wajawazito kujifungua.
Kaimu Meneja wa kanda ya Magharibi wa Benki ya NMB, Gadiel Sawe alisema kuwa misaada hiyo imetolewa kwa halmashauri za wilaya Kigoma na Manispaa ya Kigoma Ujiji ikiwa ni sehemu ya faida ambayo Benki hiyo imepata na hivyo kurudisha kwa jamii ambapo misaada hiyo imekabidhiwa kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na serikali za mitaa, Zainabu Katimba kwa niaba ya halmashauri hizo.
Sawe aliitaja misaada iliyokabidhiwa kuwa ni vitanda 10 vya kujifungulia wajawazito, vitanda vitano vya kulalia wagonjwa, viti vitano vya kubebea wagonjwa (Wheel Chair) na seti 500 za vifaa wanavyotumiwa na wajawazito wanapojifungua ambavyo vyote vimetolewa kwa halmashauri ya manispaa ya Kigoma huku Benki hiyo ikitoa vitanda 50 vyenye uwezo wa kulala watu 100 kwa shule maalum ya Bitale Halmashauri ya wilaya Kigoma.
Akipokea misaada hiyo kwa niaba ya halmashauri hizo za mkoa Kigoma, Naibu Waziri wa TAMISEMI,Zainabu Katimba alisema kuwa wadau wa maendeleo na taasisi za binafsi zimeweza kutoa misaada hiyo kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji na utendaji yaliyowekwa na serikali huku amani na usalama ikiwa msingi wa utendaji huo.
Naibu Waziri huyo alisema kuwa wakati wadau wa maendeleo wakiunga mkono huduma za afya mkoani Kigoma, serikali ya Raisi Samia imewezesha kujengwa kwa hospitali sita za wilaya, vituo vya afya 20 na kutolewa kwa gari 10 za wagonjwa mkoani Kigoma kwa miaka minne ambayo Rais Samia yupo madarakani.
Awali Katibu Tawala wa mkoa Kigoma,Hassan Rugwa ameishukuru benki ya NMB kwa msaada iliotoa ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono serikali katika kuboresha utoaji huduma kwenye sekta ya afya na elimu mkoani Kigoma na kupunguza changamoto zilizopo kwenye utoaji huduma.
Rugwa alisema kuwa msaada huo unakuja huku Benki hiyo miezi miwili iliyopita ikiwa imekabidhi msaada wa shilingi milioni 100 katika shule ya Sekondari ya wasichana Kahimba wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ambapo Benki hiyo ilisaidia kuezeka mabati ya shule hiyo.
Mwisho.
0 Comments