Na Shomari Binda-Musoma
VIJANA wa group la Urafiki Vicoba waliopo Musoma wamekumbushwa umuhimu wa kujiwekea akiba kupitia hisa na michango mingine.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kikundi hicho Makongoro Abdi alipokuwa akizungumza na wanachama jana mei 4,2025
Amesema kujiwekea akiba ni suala la msingi kutokana na changamoto za maisha na kuwa katika umoja kunasaidia kubadilishana mawazo.
Makongoro amesema lengo la kuanzishwa kwa umoja huo ni kusaidiana kwa shida na raha na kuwahimiza wanachama kupendana na kuwa wamoja.
Amesema uwekaji wa akiba na ununuaji wa hisa utawezesha kwa baadae kupata mikopo nafuu kupitia umoja huo na kujiinua kiuchumi.
" Niwakumbushe vijana wenzangu upo umuhimu mkubwa wa kujiwekea akiba na ununuaji wa hisa ambao tunaendelea nao hivi sasa.
" Kwa kuwa ndio tunaanza umoja wetu baadae uwekezaji tunaoufanya utatusaidia kukopeshana kupitia kikoba chetu na kujiinua kiuchumi",amesema.
Mweka hazina wa kikundi hicho Joseph Misana amesema fedha za kikundi zipo salama kwa kuwa kila zinapokusanywa zinaingizwa kwenye akaunti na kila mwanachama anapata ujumbe.
Amesema fedha zinakusanywa na kutunzwa na hakuna itakayopotea na muda ukifika mikopo itatolewa kwa mujibu wa katiba inavyoelekeza.
0 Comments