Header Ads Widget

PATUTA YAWAPONGEZA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO, KIHONGOSI KWA TEUZI CCM

 




Na. Mwandishi Wetu

TAASISI ya Pamoja Tutashinda Tanzania (PATUTA) imepongeza viongozi wapya wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu CCM Taifa na Ndg. Kenani Kihongosi kwa nafasi ya Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa.

Kwa mujibu wa taarifa kwa Umma iliyotolewa Agosti 24,2025 na Katibu wa PATUTA Kanda ya Ziwa, Jamal Ally imeeleza kuwa, chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mkuu wa PATUTA, Dkt. Aiden Ndaombwa, imetoa pongezi hizo za dhati kwa viongozi hao waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi CCM walioteuliwa jioni ya Agosti 23, 2025.

Dkt. Aiden Ndaombwa amemwakikishia kushirikiana na Katibu Mkuu Dkt. Asha-Rose Migiro katika mambo mbalimbali katika ustawi wa Chama na Wananchi.

"Hongera nyingi sana! Hakika wewe ni mweledi wa ukweli, kiongozi shupavu na mfano wa kuigwa kwa watanzania wengi, hususani wanawake na vijana.

PATUTA tunaamini uteuzi huu utazidi kuimarisha uimara wa CCM, kukuza mshikamano wa kitaifa na kuongeza kasi ya maendeleo ya taifa letu" Amesema Dkt. Aiden Ndaombwa.


Aidha,  amemwelezea Ndugu Kenani Kihongosi kwa kuaminiwa na kuteuliwa nafasi hiyo mpya kwani anaamini ni mchapa kazi na mwenye bidii katika Uongozi unaoacha alama.

"Nichukue nafasi hii kukupongeza pia Kenani Kihongosi Uteuzi huu unaonesha wazi imani kubwa ya chama kutokana na umahiri, bidii na msimamo wako thabiti katika siasa na uongozi.

"PATUTA tunaamini nafasi hii muhimu itazidi kulipa chama nguvu mpya, kuongeza hamasa kwa wanachama na kuchochea maendeleo ya taifa letu" amemalizia Dkt. Aiden Ndaombwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI