Na Mwandishi wetu.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu ametangaza kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya kilichotokea asubuhi ya leo May 07,2025 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya moyo.
Akitangaza taarifa hizo leo, Rais Samia amesema “Kwa masikitiko makubwa natangaza kifo cha Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Msuya kilichotokea leo May 07,2025 saa tatu asubuhi katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya moyo, Mzee Msuya ameugua muda mrefu na amekuwa akipatiwa matibabu ndani na nje ya nchi ikiwemo Hospitali ya JKCI, Mzena na kule London Uingereza”
“Natangaza siku saba za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia May 07,2025 hadi May 13, 2025, taarifa zaidi kuhusu msiba zitaendelea kutolewa na Serikali, poleni sana Watanzania”
Mwisho.
0 Comments