Header Ads Widget

TLP YAMTANGAZA WANGIRA MGOMBEA URAIS

Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kimemchagua Yusuph Wangira, kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho huku makamo akiwa ni Amana Selemani Mzee.

Katika uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika  Wilaya ya Ubungo mkoa Dar es Salaam, wajumbe walikua ni 103 huku wagombea wakiwa watatu ambao ni  Yusuf Wangira kura 52, Neema Nyerere kura 6 na Wilson Ellas kura 46.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa chama cha cha hicho jijini hapa Mwenyekiti wa uchaguzi huo Coaster Jimmy, amesema jumla ya wapiga kura 103 na  waliopigiwa kura walikuwa watatu, Neema Nyerere alipata kura 6 , Wilson Ellas 46 na Yusuph Wangira amepata kura 52 hivyo chama hicho kimemtangaza Yusuph Wangira ndiyo atakaye kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia  TLP.

Akishukuru wanachama katika uchaguzi huo Yusuph Wangira amesema anawahakikishia ushindi wa chama chao katika uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani mikoa yote na mgombea mweza wake Amana Selemani Mzee.

Kwa upande wake Msajili Msaidizi wa vyama vya Siasa Tanzania Sisty Nyahoza ,amewapongeza Tanzania Labour Party TLP, kwa kufanya uchaguzi kwa amani wa chama hicho .

Msajili Nyahoza amesema katika uchaguzi lazima ukubali mambo mawili kushinda na kushindwa na uchaguzi wenu umeenda vizuri demokrasia imefanya kazi hivyo aliwaomba wawe wamoja kama chama wafanye kazi za chama na kuwa wastamilivu aliwapongeza walioshinda na walishindwa.

Amesema vyama vitakavyoshiriki uchaguzi unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu ambapo kuna vyama 18 na vitashiriki uchaguzi na kuwataka wadumishe amani.

Kwa upande wake mgombea nafasi ya urais ndani ya Chama hicho, Wilson Ellas  ambaye kura hazijatosha ameonesha kutoridhishwa kwa matokeo hayo ambapo amesema uchaguzi wa chama hicho siyo sahihi kwani amesema jumla ya wapiga kura ni 103 huku akidai kura zilikua 104 .


"Tulipata taarifa kuwa katika mkutano huo kumeingizwa mamluki, kura zimekua nyingi kuliko wapiga kura, hii sio haki, hapa hamna demokrasia ujanja ujanja umetumika, sikubaliani na matokeo"amesema

mwisho.

SIMULIZI CHINI ⬇️⬇️⬇️⬇️

Waumini waja juu baada Askofu kuoa wake watatu 

Hivi karibuni Askofu mmoja amezua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuwatambulisha wake zake watatu hadharani na kudai ameruhusiwa ndoa ya wake wengi kitu ambacho ni kinyume na taratibu za imani yake. 

Mchungaji Sam Mwangi, anayeongoza kanisa la Faithful Gospel Church, alisema alioa mke wake wa kwanza mwaka 1996, mke wake wa pili mwaka 2004, na mke wa tatu mwaka 2018. 

Alisema ana watoto 11 na wake zake watatu na anawapenda kwa usawa bila ubaguzi wowote kama ambavyo sehemu kubwa ya jamii ya Kiafrika imekuwa akifikiria. 

Mchungaji Mwangi alisema aliamua kuwatangaza wake zake kwa umma baada ya kushutumiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa na baadhi ya waumini wa kanisa lake. 

Alisema alitaka kusafisha jina lake na kuthibitisha kuwa hakuwadanganya wake zake. Pia alisema alitaka kuwahimiza wanaume wengine kuwa wa wazi na kuacha kuwaficha wake zao wengine.

"Mungu aliumba wanawake wengi na akawapa wanaume. Hakuna mahali popote katika Biblia ambapo Mungu anakataza mitala. Kwa kweli, mitala ni baraka kutoka kwa Mungu na inasaidia kupunguza kesi za uzinzi, talaka, na uzazi wa mama mmoja," alisema. 

"Nawasihi wanaume wote waige mfano wangu na kuoa wake wengi kadiri wawezavyo. Na ninawasihi wanawake wote kukubali wamaume zao kuoa wake wengi," alisema Mchungaji Mwangi. 

Hata hivyo, hatua yake ya kijasiri haikufaulu kwa Wakenya wengi waliojitokeza kwenye mitandao ya kijamii kuelezea hasira zao mseto na kuonyesha kutoamini kwao jambo hilo. 

Wengine walimtaja kama Nabii wa uwongo ambaye alikuwa akiwapotosha wafuasi wake na kutafsiri vibaya Biblia, huku wengine walitilia shaka maadili kama kiongozi wa kidini. 

"Hapa tunachezwa, mchungaji anawezaje kuwa na wake watatu na kujidai kuwa mtu wa Mungu? Ni mnafiki na mwongo anayetumia dini kuhalalisha tamaa na uroho wake. Anapaswa kutubu na kuomba msamaha kwa Mungu na wake zake. Anaweka mfano mbaya kwa watoto wake na waumini wake," mtumiaji mmoja wa mitandao alisema. 

"Huu ni wazimu, mwanamke anawezaje kukubali kuishi na mume mwenye wanawake wengine wawili? Anawezaje kuwa na furaha na kuridhika katika hali kama hiyo? Anajishushia tu hadhi yake, anapaswa kujiheshimu na kumwacha mwanaume huyo, anastahili kitu bora kuliko kuwa mke mwenza,” mtumiaji mwingine aliandika.

Hata hivyo, kwa msaada wa Kiwanga Doctors, waamini hao waliweza kumthibiti Askofu huyo, walifanya matambiko kwa wataalamu hao wa mitishamba na mara moja wale wake zake watatu waliona makosa yao na kuamua kuondoka kwake wote. 

Kuondoa kwa wake zake, Askofu huyo alianza kupoteza ushawishi katika jamii yake hasa pale mmoja wa wake zake kutoka hadharani na kuzungumza mambo ya ndani katika familia yao yalivyokuwa na uovu mkubwa na wa kutisha. 

Baada ya hayo yote, kwa sasa mtu huyo sio Askofu tena, ni mtu wa kawaida anayezunguka tu na barabara kila siku bila kujua nini cha kufanya. Idadi kubwa ya wakazi wa eneo hilo, wanamshukuru sana Kiwanga Doctors kwa kuweza kuthibiti tabia ya Askofu huyo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI