Header Ads Widget

PPP CENTER, REDET KUFANYA KONGAMANO KESHO

 

Na Fatma Ally Matukio Daima

Kituo cha Ubia kati Sekta Binafsi na Sekta ya Umma (PPPC) kwa kushirikiana na Taasisi ya utafiti wa masuala Demokrasia (REDET) chini ya Chuo Kikuu Cha Dar es salaam  wameandaa kongamano kwa ajili ya kujadili nafasi ya sekta binafsi na sekta ya umma kuelekea dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 .

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo,  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia (PPPC) David Kafulila, amesema moja ya majukumu ya PPPC ni kuiwezesha jamii kupata uelewa  juu ya masuala ya kisera na kisheria na mipango ya Serikali katika maeneo ya ubia 

Aidha, amesema kongamano hilo ambalo litakuwa la wazi linatarajia kufanyika Mei 27,2025 katika ukumbi wa Maktaba katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam ambapo limelenga kuwashirikisha wadau mbalimbali ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa.

"PPPC iliona ipo  haja ya kushirikiana na Taasisi ya REDET ambayo imebobea katika uendeshaji wa makongamano kwa lengo la  kuushirikisha umma zaidi,

Taasisi ya REDET imekuwa ikifanya vizuri katika shughuli za makongamano na midahalo katika miongo mingi zaidi"amesema Kafulila 

Aidha amewaomba watanzania kushiriki katika kongamano hilo ambalo ni la wazi kwa ajili ya kutoa maoni na kusikiliza ili waweze kujifunza zaidi katika kufikia maendeleo ya dira ya Tanzania 2025.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya REDET, Profesa Rwekaza  Mukandala amesema kongamano hilo litakuwa na mada ndogo zitakazowasilishwa.

Akitaja mada hizo ni pamoja 

Dola, Masoko na Uhamasishaji wa Mitaji nafasi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050.

Aidha amesema kongamano hilo litaudhuriwa na Maafisa waandamizi wa Serikali, wakuu wa makampuni ya sekta binafsi, wanazuoni na wawakilishi wa kada nyingine mbalimbali 

Profesa Mukandala amewaomba wananchi kuhudhuria kongamano hilo la wazi ili waweze kushiriki kwenye mjadala kuhusu dhana ya PPP Center na nafasi yake kwenye kutekeleza Dira ya Taifa 2050.

Amesema katika mada hizo Mkurugenzi wa PPPC, David Kafulila atafanya wasilisho kuhusu dhana ya PPP Center na nafasi yake kuelekea Dira ya Taifa 2050 na Mwenyekiti wa REDET, Profesa Rwekaza Mukandala, ataongoza kongamano hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI