Header Ads Widget

RAIS SAMIA ALIPA BIL 539 UKAMILISHAJI DARAJA LA JP MAGUFULI, MRADI WAKAMILIKA ASILIMIA 99



NA MATUKIO DAIMA MEDIA,DODOMA

Wakati Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiingia madarakani mwaka 2021, ujenzi wa daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi) mkoani Mwanza ulikuwa umefikia takribani asilimia 25 na kutokana changamoto za kutetereka kwa uchumi wa dunia baada ya janga la Uviko 19, hivyo kuwa na wasiwasi wa upatikanaji wa fedha.

Hata hivyo serikali amekamilisha malipo yote ya Shilingi Bilioni 539.28 kwa ajili ya kukamilisha mradi huo kama ilivyopangwa.


Waziri wa ujenzi Mhe Abdallah Ulega ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 5 Mei 2025 wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya ujenzi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 bungeji Jijini Dodoma.

Amesema kuwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Suluhu Hassan si tu amelipa fedha zote hizo kwa mkandarasi kwa wakati, lakini amekamilisha mradi wa ujenzi uliokuwa ndoto ya mtangulizi wake Hayati Dkt John Pombe Magufuli.

Mradi huo sasa umekamilika kwa asilimia 99 na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa tukio hilo muhimu kwa Watanzania, hususani wananchi wa Kanda ya Ziwa, la uzinduzi rasmi wa Daraja la JP Magufuli au kwa jina lingine Kigongo Busisi.

Waziri Ulega amesema kuwa kukamilika kwa daraja hilo kutakuwa faraja kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa  ambao wamekuwa wakitumia muda wa takribani masaa mawili (2) kuvuka kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine. Baada ya daraja kukamilika muda wa kuvuka unatarajiwa kupungua kufikia wastani wa dakika tatu (3). Aidha, daraja hilo linategemewa kuongeza shughuli za kiuchumi ndani na nje ya mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchi jirani.

Amesema kuwa daraja hilo pia litakuwa mojawapo ya alama na fahari ya taifa letu kwani kwa urefu wake wa kilomita 3.2, litakuwa ni daraja lefu zaidi katika ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki na Kati.

Pia, Waziri Ulega awaeleza wabunge kuwa vivuko vyote vilivyokuwa vinatumika katika eneo la Kigongo – Busisi sasa vitapelekwa katika maeneo mengine nchini ambayo yana uhitaji.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI