Header Ads Widget

MDUDE APATA NAFUU: POLISI WATOA TAARIFA INAYOTIA MOYO KWA WAFUASI WAKE

 


Jeshi la Polisi nchini Tanzania limejitokeza wazi kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya uchunguzi juu ya tukio la kutoweka kwa mwanaharakati maarufu, Mdude Nyagali.

Tukio hilo limezua taharuki kubwa katika jamii, hasa baada ya kusambaa kwa madai kupitia mitandao ya kijamii kwamba baadhi ya askari polisi wanahusishwa moja kwa moja na kutoweka kwa mwanaharakati huyo.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (DCP) David Misime, jeshi hilo limepokea tuhuma dhidi ya askari wake wawili, wakihusishwa na kitendo hicho.

Taarifa zinaeleza kuwa kuna raia mmoja ambaye jina lake bado linashikiliwa kwa uchunguzi zaidi, ambaye amedai kuwa askari hao walimfuata na kumtaka afanye nao kazi ya ujasusi, wakimuahidi kumpa fedha kama malipo.

Katika kuchukua hatua za haraka, Jeshi la Polisi kupitia ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) limeunda kikosi kazi maalum.

Kikosi hicho tayari kimewasili mkoani Mbeya, eneo ambalo tukio hilo linaaminika kutokea, kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kina.

Kamishna Misime amesema kuwa Jeshi la Polisi linachukulia suala hilo kwa uzito mkubwa, na kwamba hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayebainika kuhusika, bila kujali wadhifa wake.

Amesisitiza kuwa uchunguzi utaendeshwa kwa haki, uwazi, na kwa kuzingatia sheria za nchi.

Aidha, Polisi wametoa wito kwa wananchi wote wenye taarifa zozote zitakazosaidia katika uchunguzi huu, wajitokeze na kushirikiana na vyombo vya dola.

Ushirikiano wa wananchi umeelezwa kuwa ni nyenzo muhimu katika kufanikisha uchunguzi huu na kuhakikisha haki inatendeka.

Tukio la kupotea kwa Mdude limeibua hisia kali kwa umma, hasa ikizingatiwa historia yake ya kuwa sauti ya ukosoaji wa serikali.

Watu wengi mitandaoni wameonyesha wasiwasi na hasira, wakitaka ukweli ujulikane na hatua zichukuliwe haraka.

Kwa sasa, macho ya Watanzania yameelekezwa kwa Jeshi la Polisi, wakisubiri matokeo ya uchunguzi huo. Je, ni kweli askari polisi walihusika?


SIMULIZI CHINI 👇👇


Wanandoa wararuana baaada ya kutazamwa na jicho ovu 

Bila shaka umewahi kuhisi kuwa mtu fulani anakutakia mabaya au bahati mbaya maishani mwako kwa siri?, au umewahi kupata mabadiliko ya ghafla katika afya, mahusiano au jambo ambalo ni bahati yako?.  

Ikiwa jibu lako ni ndiyo kwa maswali yoyote hapo juu, basi unaweza kuwa mwathirika wa jicho baya, mtazamo mbaya ambao unaweza kusababisha madhara kwa mtu yeyote anayeupokea.

Katika makala haya, tutashiriki nawe hadithi ya kweli ya familia moja huko Katavi ambayo waliteseka kutokana na athari za jicho baya na jinsi walivyoweza kuondokana na masaibu hayo. 

Steven Ngetich na Naomi walioana kwa furaha na wakaishi Katavi na binti yao mrembo, walikuwa na maisha mazuri, kuanzia fedha nyingi na uhusiano wenye upendo wa dhati kabisa. 

Watu wengi waliwaonea wivu, hasa majirani zao wa karibu ambao hawakuwa na furaha na pia wasio na watoto. Majirani walifanya urafiki nao na wao wakawatenda mambo mengi mema. 

Hata hivyo, nia yao majirani hao ilikuwa mbaya, waliionea jicho baya familia ya Ngetich, walifanya hivyo kwa kuchora mchoro fulani sebuleni kwao ambao ulionekana ni kitu cha kawaida lakini ilikuwa ni hila. Punde Steven na Naomi walianza kugombana, huku matatizo ya kiafya na ya kifedha yakianza. 

Wenzi hao waliokuwa na furaha mara moja walianza kubishana kuhusu mambo madogo ambayo hayakuwa mzozo hapo awali. Miongoni mwa mambo yaliyoanza kuwagombanisha ni iwapo watapata mtoto wa pili au la. Mada ikawa moto moto na kupelekea kupigana ngumi.

"Sikutaka mtoto mwingine kabisa, hapo awali, nakumbuka, hata kabla ya kufunga ndoa, tulikubaliana kwamba tutakuwa na watoto watatu lakini kuna kitu kilikuja juu yangu, sikutaka kuwa baba tena. Mke wangu alitaka mtoto haraka iwezekanavyo, na hivyo tukapigana,” alisema Steven. 

Hawakujua kuwa mchoro ule na moja ya zawadi ya jirani yao ndio chanzo cha matatizo hayo, licha ya kufanya jitihada mbalimbali ikiwa ni pamoja kuwasiliana na wazazi wao, bado mambo yaliendelea kuwa magumu kwao.  

Lakini mwisho wa siku walikuja kubaini wapi lilipo tatizo na kupata ufumbuzi baada ya kukutana na Kiwanga Doctors ambao waliwasaidia kuwapa dawa ambayo iliondoa athari za jicho baya katika maisha yao. 

Hivyo mara moja hali ilikuwa shwari, mke wa Steven Naomi aliweza kubeba mimba ya mtoto wao wa pili kama walivyokuwa wamepanga tangu awali, huku Kiwanga Doctors pia wakiwapa dawa ya kumlinda mtoto huyo dhidi ya jicho baya. 

Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio, uponyaji na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba  +255 763 926 750 au tembelea tovuti yao, maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi. 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI