Header Ads Widget

MADAKTARI BINGWA 38 WA RAIS SAMIA WAWASILI MKOANI NJOMBE

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Serikali mkoani Njombe imewataka watumishi wa afya wa mkoa huo kujitoa na kufanya kazi kwa ukaribu mkubwa na madaktari bingwa waliofika katika mkoa  kwa lengo la kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi.

Wito huo umetolewa na katibu tawala mkoa wa Njombe Judica Omary ofisini kwake mara baada ya kupokea timu ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia inayozunguka nchi nzima kwa ajili ya kutoa huduma za Kibingwa.

Dkt.Robart Masele ni kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Njombe anasema mkoa   umeendelea kunufaika na timu ya madaktari bingwa na bingwa bobezi ikiwemo kuwajengea uwezo watumishi ambapo kwa sasa wamefanikiwa kupokea jumla ya madaktari 38 watakaokwenda kwenye halmashauri zote sita  za mkoa wa Njombe.

Paskalina Endrew ni mratibu wa zoezi la madaktari bingwa awamu ya tatu kwa mkoa wa Njombe akitokea Wizara ya Afya Idara ya afya uzazi mama na mtoto anasema lengo lao ni kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi ili kupunguza changamoto ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma.

Akizungumza kwa niaba ya madaktari waliofika mkoani Njombe,Dkt James Msigwa ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya Pua,Maskio na Koo anasema katika siku sita watakazokuwepo mkoani Njombe wanayo matarajio makubwa ya kutoa huduma bora kwa wananchi wengi watakao kutana nao.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI