Header Ads Widget

KUNDO ATANGAZA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BARIADI VIJIJINI.



Na Costantine Mathiasi, Bariadi.


MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew amesema kuwa endapo Jimbo la Bariadi lenye kata 31 litagawanywa, Yeye (Mhandisi Kundo) atagombea nafasi ya Ubunge kupitia Jimbo la Bariadi Vijijini.


Kundo ameyasema hayo leo wakati akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020/2025 kwa Wajumbe wa Mkutano wa Mkuu wa CCM wilaya ya Bariadi uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Bariadi Alliance mjini Bariadi.


"Kuna Mkakati wa kukata Jimbo na Tume Huru ya Uchaguzi imepita kukusanya maoni na tumetoa mapendekezo ya Kugawa Jimbo la Bariadi lenye kata 31 ili kuwa na majimbo mawili la Bariadi mjini na Vijijini ili kurahisisha shughuli za Maendeleo na kuwasogezea huduma wananchi..." Amesema na kuongeza.


"Endapo Rais ataridhia kukata Jimbo la Bariadi na kuwa majimbo mawili, mimi (Mhandisi Kundo) nitagombea Jimbo la Bariadi Vijijini nilikotoka sababu nimezaliwa huko na mkataa kwao ni mtumwa".


Mwisho.












Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI