Header Ads Widget

BARIADI WAMPA TUZO YA HESHIMA RAIS DK. SAMIA


MBUNGE wa Jimbo la Bariadi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew (kushoto) akimkabidhi tuzo ya Heshima kutoka kwa Wana Bariadi Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Leila Ngozi kwa niaba ya Rais Dk. Samia.


Na Costantine Mathias, Bariadi.


MBUNGE wa Jimbo la Bariadi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew, kwa niaba ya wananchi wa Jimbo hilo amekabidhi zawadi ya Tuzo ya shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na kuwaletea Miradi mingi ya Maendeleo katika Jimbo la Bariadi.


Tuzo hiyo imetolewa leo (May 4, 2025) katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM jimbo la Bariadi wakati wa Uwasilishaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa Kipindi cha Miaka Mitano 2020 - 2025.


Akipokea tuzo hiyo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Leila Ngozi amesema kujitokeza kwa wingi kwa Wana Bariadi katika Mkutano huo ni kumweshimisha Rais Samia maana ishara wameziona hapo na kwamba wanaomuunga mkono Mhandisi Kundo ndio haohao wanaomuunga mkono Dk. Samia.



Mwisho.









Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI