Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Bw. Shaaban Kissu kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo, Jumatano, Mei 7, 2025, na Katibu wa Rais, Bw. Waziri Salum, wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyowakutanisha Rais Samia na wanahabari walioshiriki katika tuzo za Samia Kalamu Awards.Bw. Kissu, ambaye awali alikuwa Mkurugenzi wa Africa Media Group, alipokea taarifa ya uteuzi huo akiwa mshereheshaji wa hafla hiyo. Katibu wa Rais alisema uteuzi huo umetangazwa rasmi leo na hata Kissu mwenyewe hakuwa na taarifa kabla ya kutangazwa kwake.
“Hii taarifa nafikiri ni ‘surprise’ hata kwa Kissu mwenyewe, kwa sababu hakuwa na taarifa. Hata mmeona nimechelewa kufika hapa – tulikuwa tunashughulikia masuala hayo,” alisema Waziri Salum, akimwakilisha Rais Samia katika hafla hiyo.
Uteuzi huu unatajwa kuwa sehemu ya juhudi za kuimarisha mfumo wa mawasiliano Ikulu, sambamba na kuleta uzoefu mpya katika kusimamia mahusiano kati ya taasisi ya Urais na vyombo vya habari.
0 Comments