Header Ads Widget

MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA KIBORILONI - TSUDUNI - KIDIA UNAENDELEA KATIKA KATA YA OLDMOSHI MASHARIKI.



Na WILLIUM PAUL, MOSHI. 


MRADI wa ujenzi wa Barabara ya Kiboriloni - Tsuduni  - Kidia kwa kiwango cha lami unaendelea katika Kata ya Oldmoshi Mashariki ambapo ujenzi  wa mitaro ya kuchepusha maji ya mvua uko katika mkataba wa ujenzi. 


Mradi huu unaendelea, na zaidi ya Shilingi bilioni 3 zimetumika ambapo mradi huu wa kimkakati utasaidia wananchi kusafirisha mazao ya kilimo.



Pia utasafirisha watalii wanaopanda Mlima Kilimanjaro kupitia njia ya watu maarufu (VIP - ROUTE) kupitia geti la KIDIA.


Wananchi wameishukuru Serikali kwa kufadhili Mradi huo pamoja na juhudi za Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Prof. Patirck Ndakidemi na Diwani wa Kata ya Old Moshi Mashariki, Jane Mandara kwa kupigania mradi huo wa kielelezo kwa wananchi wa Kata hiyo. 



Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI