mjumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa kupitia wilaya ya Iringa mjini Islam Huwel (kulia) akiwa na mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa anayewakilisha wilaya ya Iringa vijijini Arif Abri picha na Matukio Daima Media
NA MATUKIO DAIMA MEDIA
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kupitia Wilaya ya Iringa Mjini, Islam Huwel, amepongeza kasi kubwa ya ujenzi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini, akieleza kuwa hatua hiyo ni ushahidi wa dhamira ya dhati ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli.
Akizungumza na Matukio Daima Media Huwel alisema kila Mtanzania kwa sasa anaweza kuona na kushuhudia miradi mikubwa inayotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali ya nchi, hali inayothibitisha kuwa serikali imejipanga ipasavyo katika kuinua maisha ya wananchi.
“Tunaona kasi kubwa ya ujenzi wa miradi ya maendeleo nchini, na sisi wananchi wa Iringa Mjini pia hatujabaki nyuma. Miradi ya barabara, elimu, afya, maji na miundombinu ya kijamii inaendelea kwa kiwango kikubwa kuwa hata wapinzani wananufaika na miradi hii, jambo linaloonesha kuwa serikali ya Rais Samia haibagui bali inalenga maendeleo ya wote,” alisema Huwel.
Huwel alibainisha kuwa hatua ya serikali kutekeleza miradi hiyo kwa vitendo imesaidia kuimarisha heshima ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mbele ya wananchi, kwa kuwa wanachokisikia kwenye Ilani ya uchaguzi sasa wanakiona kwa macho.
“Ilani ya CCM haibaki kwenye makabrasha au maneno ya kampeni pekee leo hii wananchi wanaona jinsi ilivyogeuka kuwa vitendo ni madaraja, ni vituo vya afya, ni shule, ni maji safi, ni barabara yote haya ni matokeo ya uongozi mahiri wa Rais Samia,” aliongeza.
Kwa mujibu wa Huwel, serikali ya awamu ya sita imekuwa ikisikiliza maoni ya wananchi, kushirikiana nao bega kwa bega, na kujibu changamoto kwa haraka alisema kuwa hii ni serikali ya wananchi na inafanya kazi kwa ajili ya watu.
Hata hivyo Huwel aliwataka wananchi wa Iringa na Tanzania kwa ujumla kutambua mchango mkubwa wa Rais Samia na serikali yake kwa kuwazawadia kura nyingi katika uchaguzi ujao ili aweze kuendeleza mafanikio yaliyopatikana na kuongeza kasi ya maendeleo.
“Zawadi kubwa kwa Rais Samia si maneno pekee ya shukrani, bali ni kura za kutosha. Tuonyeshe kuthamini kazi yake kwa kuendelea kumpa ridhaa ya kuongoza tunahitaji maendeleo zaidi, tunahitaji miradi mikubwa zaidi, na haya yote yatatimia kwa kumuunga mkono kwa dhati,” alisema.
Huwel pia alishauri viongozi wa chama kuendelea kuwa karibu na wananchi, kusikiliza matatizo yao na kuhakikisha kwamba wanawasaidia kufikia huduma bora zinazotolewa na serikali.
kwani alisema kuwa kazi kubwa imefanyika, lakini bado yapo maeneo yanayohitaji msukumo zaidi, hivyo ushirikiano wa viongozi, wanachama na wananchi wote ni muhimu.
“Tuendelee kushirikiana. Tushirikiane katika kulinda haya mafanikio tushirikiane kuiunga mkono serikali yetu na chama chetu cha CCM Kwa pamoja tutafikia Tanzania ya viwanda, uchumi wa kati na maisha bora kwa kila Mtanzania,” alihitimisha.
0 Comments