Header Ads Widget

HAMAS YASEMA 'HAKUNA MAANA' YA MAZUNGUMZO WAKATI ISRAEL IKIPANGA KUPANUA OPERESHENI GAZA

 

Afisa mkuu wa Hamas amesema "hakuna maana" ya mazungumzo zaidi kuhusu mpango mpya wa kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka Gaza baada ya Israel kusema kuwa itapanua mashambulizi yake ya ardhini na kuikalia Gaza kwa muda usiojulikana.

Bassem Naim alidsema kuwa kundi linalojihami la Palestina halitajihusisha na mapendekezo mapya huku Israel ikiendelea na kile alichokiita "vita vya njaa".

Israel inasema lengo lake ni kuwarejesha mateka ambao bado wanashikiliwa na Hamas.

Maafisa wa Israel walisema siku ya Jumatatu kuwa mipango hiyo inahusisha kuwahamisha watu wengi zaidi ya milioni 2.1 wa Gaza, kuteka eneo lote, na kudhibiti misaada ya kibinadamu baada ya kizuizi cha miezi miwili.

Pia walisema mashambulizi hayo hayataanza hadi baada ya ziara ya Rais wa Marekani Donald Trump katika eneo hilo wiki ijayo, na kuwapa Hamas kile walichokiita "dirisha la fursa" kufikia makubaliano.

Uingereza, Ufaransa na Umoja wa Mataifa wamekosoa mipango mipya ya Israel.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alielezea wasiwasi wake na kuonya kwamba "itasababisha raia wengi zaidi kuuawa na uharibifu zaidi Gaza".

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wao pia wamelaani pendekezo la Israel la kuwasilisha misaada kupitia makampuni ya binafsi katika vituo vya kijeshi, wakisema kuwa itakuwa ni ukiukaji wa kanuni za msingi za kibinadamu na kwamba hawatatoa ushirikiano.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI