Na Shomari Binda-Tarime
WAKANDARASI wanaokusudiwa kutekeleza miradi 19 ya maendeleo kwenye vijiji mbalimbali kwenye jimno la Tarime Vijijini wameonyeshwa maeneo ya utekelezaji.
Ziara iliyofanyika april 9,2025 iliyowahusisha wataalam na ofisi ya mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini imeshiriki huku lengo ikiwa kuanza utekelezaji wake mara moja.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya mbunge imesema maeneo yaliyofikiwa ni pamoja na Nyarokoba Kijiji cha Msenge ambapo kuna ujenzi wa jengo la utawala shule ya msingi Musege pamoja na nyumba ya mwalimu.
Eneo la pili lililofikiwa ni Kata ya Gorong'a Kijiji cha Kenyamsabi ambapo kuna ukamilishwaji wa zahanati ya Kijiji hicho pamoja na Kijiji cha Nyanungu ambapo pia kuna ujenzi wa zahanati.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo kutoka ofisi ya mbunge Kata ya Itiryo Kijiji cha Kangariani pia kimefikiwa kikiwa na ujenzi wa nyumba ya mtumishi na zahanati.
Ujenzi wa jengo la kufulia na njia za kupita wagonjwa kituo cha afya Magoma Kijiji cha Magoma kimefikiwa na ziara hiyo ili kufanyika utekelezaji.
Katibu wa mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini Remmy Mkapa amezungumzia ziara hiyo na kusemea ni miradi mingi kwa wakati mmoja inayokwenda kutekelezwa.
Ameseema maeneo mengine waliyoonyeshwa wakandarasi ni Kata ya Matongo Kijiji cha Matongo ambapo kuna ujenzi wa nyumba 1 ya mtumishi shule ya msingi Matongo na jengo la utawala.
" Maeneo 19 ya utekelezaji wa miradi wameonyeshwa wakandarasi ambayo utekelezaji wake unakwenda kuanza Mara moja.
" Pale Kata ya Matongo pia tumefika Kijiji cha Nyangoto ambapo kuna ujenzi wa nyumba pacha ya watumishi shule ya msingi Nyamongo",amesema.
Amesema maeneo mengine ya ujenzi wa miradi yaliyofikiwa ni Mbogi,Pemba,Gwitiryo,Regicheri pamoja na Kata ya Susuni.
Katibu huyo amewaomba wananchi na wadau wa maendeleo ya Tarime vijijini kushirikiana kuijenga Tarime Vijijini.
Aidha katibu huyo ametoa shukrani kwa Mheshimiwa Chief Mwita Waitara Mbunge wa Jimbo la Tarime vijijini kwa ufuatiliaji wa vitendo wa miradi hii ya maendeleo
0 Comments