Na Shomari Binda-Butiama
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Fadhil Maganya ameonya wanaotarajiwa kugombea udiwani na ubunge kuacha kuwasingizia viongozi kuwa wamewatuma kugombea.
Onyo hilo amelitoa leo aprili 9,2025 kwenye kilele cha wiki ya wazazi kwa mkoa wa Mara iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kanisa Katoriki Wilaya ya Butiama.
Katika maadhimisho hayo yaliyoambatana na kongamano lililohusu elimu,malezi,maadili,mazingira na utamaduni.
Amesema zipo taarifa za wanaotaka kugombea kupita kwa wanachama na kudai wametumwa na viongozi wa kitaifa jambo ambalo sio kweli.
Maganya amesema sio jambo zuri na jema kuwasingizia viongozi juu ya suala hilo bali muda ukifika kila mmoja anayo nafasi ya kujitokeza naa kugombea.
Amesema Chama cha Mapinduzi kinayo hazina kubwa ya wanachama wanaoweza kujitokeza na kuomba nafasi za uongozi kwa kuwa wana sifa zote.
" Tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu na kupitia kongamano hili la wiki ya wazazi hapa Butiama kutoa onyo kwa wale wote wanaodai kutumwa na viongozi kuhombea udiwani au ubunge.
" Huo ni uongo na tusiwasikilize kila mmoja anayo nafasi ya kujitokeza kuomba nafasi za uongozi na kuacha kuwasikiliza wale wanaosema wametumwa na viongozi",amesema
Aidha Mwenyekiti huyo amemuomba Katibu wa CCM mkoa wa Mara kuwachukulia hatua wale wote wanaokwenda kinyume na miongozo ya chama.
Akizungumzia yaliyojitokeza kwenye mjadala wa kongamano hilo Mwenyekiti huyo amewataka wazazi na walezi kusimamia maadili ya watoto na hata wanachama wa jumuiya wazingatie maadili kwa mujibu wa kanuni.
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Taifa Mgore Miraji amesema kama maadili yatasimamiwa vizuri hakuna mtoto atakayekuwa na maadili mabovu
Mgore amesema mmomonyoko wa maadili umekuwa mkubwa kwenye jamii na kama hali hiyo ikiwndelea kuachwa hali itakuwa mbaya zaidi na kuiomba jumuiya ya wazazi mkoa wa Mara kuendelea kusimamia.
0 Comments