Header Ads Widget

TUNDU LISSU AFIKISHWA MAHAKAMANI ASOMEWA SHITAKA LA UHAINI NA KUCHAPISHA TAARIFA ZA UONGO

 


TAZAMA VIDEO LISSU AKIFIKISHWA MAHAKAMANI BOFYA LINK HII

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shitaka moja la uhaini.


Lissu amefikishwa mahakamani hapo leo Aprili 10, 2025 saa 10: 15, huku Wakili Nassoro Katuga akimsomea shitaka hilo.


Upande wa utetezi unaongozwa na Wakili Dk Rugemeleza Nshalla, Hekima Mwasipu, Jebra Kambole, Dickson Matata, Gastoni Garubindi na Michael Lugina.


Mwanasiasa huyo alikamatwa jana Aprili 9, 2025 wilayani Mbinga mkoani Ruvuma muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara na kusafirishwa hadi Dar es Salaam. Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Lissu alihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Central jijini Dar es Salaam.



Pia Tundu Lissu katika Mahakama hiyo amesomewa kesi ya pili yenye mashitaka matatu ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa X.

 katika kesi nyingine alipandishwa kizimbani na kusomewa shitaka moja la uhaini, huku kesi hiyo ikipangwa kuendelea Aprili 24, 2025.

Lissu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shitaka moja la uhaini leo saa 10.15 jioni. Upande wa utetezi unaongozwa na Wakili Dk Rugemeleza Nshalla, Hekima Mwasipu, Jebra Kambole, Dickson Matata, Gastoni Garubindi na Michael Lugina.

Mwanasiasa huyo alikamatwa jana Aprili 9, 2025 wilayani Mbinga mkoani Ruvuma muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara na kusafirishwa hadi Dar es Salaam. Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Lissu alihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Central jijini Dar es Salaam.


Taarifa zaidi endelea Kufuatilia mitandao yetu ya kijamii pamoja na chanel ya Matukio Daima Tv 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI