Header Ads Widget

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE: ARSENAL YAMTAKA KINGSLEY COMAN

 

Coman

Arsenal wamewasiliana na Bayern Munich kuulizia upatikanaji wa winga Kingsley Coman, mwenye umri wa miaka 28. (Sky Sports)

Eintracht Frankfurt wanataka ada ya takriban €100milioni (£86.3m) kwa mshambuliaji Hugo Ekitike, mwenye umri wa miaka 22, huku Arsenal na Tottenham wakionyesha nia ya kumsajili. (Bild - in German)

Tottenham wako tayari kuvunja rekodi yao ya usajili na kulipa takriban £65m kumsajili mshambuliaji wa Wolves Matheus Cunha, mwenye umri wa miaka 25. (Fichajes - in Spanish)

Crystal Palace wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 27, kufuatia mafanikio yake kwa mkopo akiwa Aston Villa. (Sun)

Rashford

Liverpool na Everton wanatarajiwa kushindana kumsajili kiungo wa Sunderland Chris Rigg, mwenye umri wa miaka 17, majira ya kiangazi. (The i)

Manchester United hawatarajiwi kumuuzia kipa Andre Onana, mwenye umri wa miaka 29, majira haya ya joto isipokuwa kama dau kubwa la faida kutokana na ada ya £47m waliyolipa litawekwa mezani (NBC Sports)

Hata hivyo, United wamepunguza bei ya kumuuza mshambuliaji Alejandro Garnacho, mwenye umri wa miaka 20, kutoka zaidi ya £50m hadi chini ya £40m ili kurahisisha mauzo. (Tutto Mercato Web)

United wanaonyesha nia ya kumsajili kijana wa Ajax Abdellah Ouazane, mwenye umri wa miaka 16, baada ya kung'ara akiwa Morocco kwenye mashindano ya U17 Africa Cup of Nations. (Daily Mail)

Erling Haaland

Manchester City watamuongeza mkataba wa mwaka mmoja kiungo Ilkay Gundogan, mwenye umri wa miaka 34, na kumbakiza hadi mwaka 2026. (Fabrizio Romano)

Real Madrid watajaribu kumsajili mshambuliaji wa City Erling Haaland, mwenye umri wa miaka 24, iwapo Vinicius Jr ataondoka na kuelekea Saudi Arabia kama inavyodaiwa. (Sky Sports)

Barcelona wameweka dau la thamani ya £78m kwa winga Raphinha, mwenye umri wa miaka 28, kufuatia uvumi wa kuvutiwa na klabu za Saudi Pro League. (Catalunya Radio)

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI